Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MCHANGO WA MAANDISHI WA NDG KABWE ZUBERI ZITTO, MB KUHUSU BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA WA FEDHA 2014/2015

MCHANGO WA MAANDISHI WA NDG. KABWE
ZUBERI ZITTO, MB KUHUSU BAJETI YA
SERIKALI YA MWAKA WA FEDHA 2014/2015
Mheshimiwa Spika, Kwanza kabisa napenda
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa
nguvu za kuweza kuandika mchango wangu
huu mdogo kwenye mjadala wa Bajeti ya
Serikali mwaka 2014/15. Kama wengi
mnavyofahamu mnamo tarehe 1 Juni mwaka
2014 nilimpoteza mama yangu mzazi na
kumsitiri siku iliyofuata tarehe 2 Juni, 2014.
Huu ni msiba mkubwa sana kwangu na ndugu
zangu wote kwani mama yetu Bi. Shida Salum
alikuwa nguzo katika familia. Nafahamu kuwa
jamaa na marafiki wa mama pia wamepoteza
mtu wao muhimu sana. Napenda kuwashukuru
nyote kabisa kwa salamu zenu za pole kwetu.
Sina namna ya kuelezea shukrani zangu kwenu
kwani Bi Shida kwangu alikuwa zaidi ya mama
mzazi, alikuwa rafiki, dada na nguzo.
Ninamshukuru Allah kwa kuniwezesha
kumwuguza na kumsitiri mama yangu. Hakuna
amali kubwa ambayo Mungu amenipa zaidi ya
hiyo. Nawashukuru tena nyote kabisa wabunge
wenzangu kwa kushirikiana nami kwa namna
zozote zile kumwuguza na kumsitiri mama
yangu. Mungu atawalipa malipo
yanayowastahili kwa amali na vitendo vyenu.
Sisi kama familia tutaendelea kumwombea dua
mama yetu na kumtolea sadaka ili ahifadhiwe
mahala pema.
Mheshimiwa Spika, ningependa niwe nanyi
katika mjadala huu muhimu wa kila mwaka wa
Taifa letu. Hata hivyo bado Mungu
hajaniwezesha nguvu za kusimama na
kuzungumza. Pindi nitakapowezeshwa nguvu
hizo nitakuwa nanyi kwa kipindi hicho
nitakachojaaliwa ili kushiriki katika kazi za
kuendeleza Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii
kumpongeza Waziri wa Fedha ndugu Saada
Salum kwa kuwasilisha Bajeti yake ya kwanza
kabisa kama Waziri wa Fedha wa pili
Mwanamke wa nchi yetu. Nampongeza kwa
kuchukua hatua kadhaa za kuboresha
usimamizi wa fedha za umma na hasa
matamko aliyotangaza ya kupambana na
misamaha ya kodi ambayo imeongezeka
mpaka kufikia asiliamia 3.5 ya Pato la Taifa na
asilimia 10 ya Bajeti ya Serikali. Misamaha ya
Kodi mwaka 2012/13 ilifikia tshs 1.5 trilioni
ambayo ni sawa na asilimia 15 ya makusanyo
yote ya ndani na ni sawa na takribani fedha
zote za kodi ambazo Serikali ilikusanya kama
kodi ya mishahara ya Wafanyakazi (PAYE).
Hata hivyo, matamko ya Serikali yana
mapungufu makubwa sana na ni matamko yale
yale yanayorudiwa kila mwaka bila utekelezaji.
Kuweka wazi misamaha ya kodi na watu au
asasi zilizofaidika na misamaha hiyo ni hatua
nzuri lakini haitoshi kama hatua hiyo
haitaendana na kufanya ukaguzi wa misamaha
hiyo. Kamati ya Bunge ya PAC ilitoa agizo
mwaka 2013 la kutaka Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali kukagua
misamaha ya kodi kama matumizi mengine
yeyote ya Serikali. Ieleweke kwamba misamaha
ya kodi ni ruzuku (subsidy), ni fedha ya Serikali
ambayo iwapo ingekusanywa ingekaguliwa kwa
mujibu wa sheria. Matamko ya Serikali ya
kuweka wazi misamaha lazima yaendane na
kuifanyia ukaguzi (auditing) na kuweka wazi
matokeo ya ukaguzi huo. Vilevile ni lazima sasa
katika Sheria ya Fedha ya mwaka 2014/15
kuweka kipengele cha kuzuia misamaha ya
kodi kuzidi asilimia moja ya Pato la Taifa na
kurekebisha Sheria ya Ukaguzi ya umma wa
mwaka 2008 ili kumpa mamlaka ya kisheria
CAG kukagua misamaha ya kodi na kuweka
wazi matokeo ya ukaguzi huo kwa umma.
Kodi kwa Wafanyakazi
Mheshimiwa Spika, Waziri wa Fedha
ametangaza nafuu ya kodi kwa wafanyakazi wa
kima cha chini kutoka kiwango cha 13% mpaka
12%. Kiwango hiki ni kidogo mno na
hakimsaidia mfanyakazi kubakia na fedha kwa
ajili ya matumizi yake na pia kwa ajili ya
kujiwekea akiba. Ni dhahiri kuwa PAYE ni
chanzo kikubwa sana cha mapato ya ndani ya
Serikali. Kwa mfano mwaka 2013/14 Serikali
ilitarajiwa kukusanya tshs 1.5 trilioni kama
PAYE ambapo tshs 1 trilioni kutoka idara ya
walipa kodi wakubwa na tshs 500 bilioni kutoka
idara ya kodi za ndani. Hata hivyo, utaona
kuwa mapato haya ni sawa sawa na kodi
inayosamehewa kupitia misamaha ya kodi
hivyo iwapo misamaha ya kodi ikipunguzwa
mpaka kiasi cha asilimia 1 ya Pato la Taifa,
Serikali itakusanya kodi ya kutosha kuzipa
pengo la punguzo la kodi kwa wafanya kazi.
Vile vile Serikali inapoteza kodi nyingi sana
kupitia ukwepaji kodi unaofanywa na
makampuni makubwa ya kimataifa
yanayowekeza hapa nchini (tax evasion and tax
avoidance) kwa kiwango cha asilimia 5 ya Pato
la Taifa. Iwapo Serikali itajiunga na mikataba ya
kimataifa ya kupambana na ukwepaji kodi na
pia kuimarisha kitengo cha kodi za Kimataifa ili
kupambana na Multinational Corporations
ambao wanatumia njia mbalimbali kuhamisha
faida zao nje, kutangaza hasara hapa nchini na
kukwepa kodi za thamani ya zaidi ya shilingi
trilioni mbili kila mwaka kwa mujibu wa
takwimu za Global Financial Integrity.
Napendekeza kuwa kiwango cha chini cha
kipato (mshahara) kukatwa kodi kiwe shilingi
330,000 na kiwango cha chini cha kodi kiwe
asilimia 9 tu.
Mheshimiwa Spika, Kiwango hiki cha kodi pia
kinawezekana kwa Serikali kuchukua hatua
dhidi ya matumizi mabovu ya Serikali. Kwa
mfano, kwa mujibu wa Taarifa ya Mkaguzi
Mkuu wa ndani wa Serikali mwaka 2013,
mfumo wa kukagua utumishi wa umma
umegundua kuwa jumla ya wafanya kazi wa
Serikali 6500 walikuwa wameajiriwa mara mbili
kwa majina yale yale, 2700 mara tatu na
kulikuwa na watumishi 2500 waliokuwa
wanachukua mishahara miwli mpaka mitatu kila
mwezi. Baada ya mfumo wa Lawson
kuanzishwa jumla ya wafanyakazi hewa 14,000
waligundulika katika jumla ya wafanyakazi
478,000 wa Serikali. Hatua ya kuondoa
matumizi mabovu kutokana na kulipa
mishahara hewa pia inaweza kusaidia
kupunguza mzigo wa kodi kwa wafanyakazi
nchini. Serikali hutumia wastani wa shilingi
bilioni 360 kila mwezi kulipa mishahara
ambapo katika hizo shilingi bilioni Kumi kila
mwezi zimekuwa zikilipwa kwa watumishi
hewa. Nafuu ya kodi kwa wafanyakazi nchini
katika sekta zote na hasa wafanyakazi wa kima
cha chini kitachochea matumizi binafsi ya
bidhaa na huduma na hivyo kuchangamsha
uchumi na kuwezesha uwekaji wa akiba nchini.
Nashauri ukaguzi zaidi ufanyike katika utumishi
wa umma ili kumaliza kabisa tatizo la
wafanyakazi hewa nchini.
Mheshimiwa Spika ninapongeza kuanzishwa
kwa kodi ya zuio kwa ada kwa Wakurugenzi
wa makampuni na Mashirika. Kodi hii
itaongeza mapato ya Serikali. Hata hivyo kodi
kama hii pia itozwe kwenye posho ambazo
viongozi wa kisiasa na watumishi wa Serikali
wanalipwa isipokuwa posho ya kujikimu (per
diem). Vile vile uamuzi wa kuagiza Wizara,
Idara na Wakala za Serikali kukusanya
maduhuli kwa kutumia mashine za kielektroniki
ni uamuzi muhimu sana ambao utaongeza
ufanisi katika ukusanyaji wa mapato yasiyo ya
kodi. Kamati ya PAC iliagiza jambo hili tangu
mwaka 2013 na ninaamini kuwa Polisi wa
Usalama barabarani wataanza kutoa ‘traffic
notifications’ kwa njia hii; pia Wizara ya Ardhi
wataanza kutoa Hati za Ardhi za kielektroniki
na kukusanya maduhuli kwa njia hii ikiwemo
Wizara ya Nishati na Madini kwa tozo
mbalimbali wanazotoza. Juhudi zote hizi lazima
zionekane kwa kupunguza mzigo wa kodi kwa
Wafanyakazi ambao kiukweli ni wachache
(takribani 1.3 milioni) lakini wanabebeshwa
mzigo mkubwa wa kodi kuliko wawekezaji
wakubwa.
Mheshimiwa Spika, Tanzania haiwezi
kuendelea kuwa nchi ambayo Serikali yake
inaendeshwa na fedha za wafanyakazi,
wafanyabiashara wadogo na wahisani. Ni
lazima makampuni makubwa ya uwezekaji
nchini yashiriki kuendesha Serikali kwa kulipa
kodi stahili na kuondoa kabisa misamaha
ambayo haina mahusiano yeyote na ukuaji wa
ajira nchini na kuongeza thamani ya mazao
yetu ya kilimo. Vile vile ni muhimu sana
kuongeza juhudi za kukuza ajira ili kuwa na
wafanyakazi wengi ambao watapelekea
kuongeza mapato ya Serikali badala ya
kukamua kundi dogo lililopo hivi sasa. Nchini
Kenya kiwango cha chini cha Kodi ya Mapato
kwa wafanyakazi (PAYE) ni asilimia 10 tu kwa
sababu idadi ya walipaji wa kodi hii wanafikia
takribani milioni kumi wakati Tanzania ina
wafanyakazi wanaolipwa mishahara ya kila
mwezi milioni 1.3 tu.
Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima
Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Hali ya Uchumi
wa Taifa inaonesha kuwa Tanzania ina jumla
wa mifuko mitano ya Hifadhi ya Jamii yenye
wanachama 1.3 milioni pekee. Idadi hii ya
wanachama ni 6% ya nguvu kazi ya Tanzania.
Hata hivyo nguvu kazi ya nchi haipo kwenye
wafanyakazi wa mishahara pekee kwani
asilimia takribani 70 ya Watanzania wanaishi
vijijini na kujihusisha na sekta ya Kilimo. Kwa
kuwa mifuko ya Hifadhi ya Jamii haijafikia
wakulima maana yake Watanzania wengi sana
wanaishi ya mashaka kwa sababu hawana
Bima ya Afya, hawana mafao mengine ya
muda mfupi na wala hawana pensheni. Hali hii
ni lazima kuirekebisha kama tunataka Taifa
lenye maendeleo. Hifadhi ya Jamii sio suala la
pensheni tu bali pia ni suala la uwekezaji wa
akiba (savings) na uwekezaji wa ndani
(investments).
Mheshimiwa Spika, Kasi ya ukuaji uchumi na
uwekezaji (Growth and investment rates) vina
mahusiano chanya.Takwimu za Penn World
Tables (2002) zinaonyesha kuwa kwa nchi 38
za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara wastani
wa ukuaji uchumi ulikuwa 0.6% na wastani wa
uwiano wa uwekezaji na ukuaji uchumi ulikuwa
10%. Kwa nchi 9 za Asia (9 Asian 'miracle'
economies), wastani

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO