Timu za Ghana na Nigeria kutoka Afrika zimefanikiwa kuitoa kimasomaso Afrika katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil kwa Ghana kutoka sare ya goli 2.2 dhidi ya miamba ya Ujerumani na Nigeria kuwafunga goli 1 kwa bila katika mechi za usiku wa jana kuamkia leo.
Wajerumani hawakuamini kilichokuwa kikifanywa na vijana wa Ghana huku mshambuliaji wao Miloslav Klose kutokea benchi na kuisawazishia Ujerumani na yeye kufikisha goli 15 katika michuano ya kombe la Dunia, rekodi ambayo ilikuwa inadhikiliwa na Ronaldo De Lima wa Brazil.
Ndugu familia ya Boateng, Prince Boateng anyechezea Ghana kushoto na kaka yake Jerome Boateng anayechezea Ujerumani Miroslav Klose akiruka sarakasi kushangilia goli lake la 15 na la kuisawazishia Ujerumani katika michuano ya Kombe la Dunia. Dede Ayew akishangilia goli la kwanza alilofunga kwa Ghana Mtifuano uwanjani ********** Nigeria na ushindi wa kwanza katika miaka 16 Timu ya Nigeria ilifanikiwa kuifunga Bosnia&Herzegovina goli moja kwa bila kupitia mchezaji Peter Odemwingie na kuweka rekodi ya kushinda mechi ya kwanza katika miaka 16 ya kombe la Dunia. Peter Odemwengie akishangilia goli lake lililowaonfosha Bosnia kwenye michuano hiyo Wachezaji wa Nigeria wakimpongeza mwenzao Odemwengie kufunga goli lililovunja rekodi ya Nigeria kukosa ushindi kwenye Kombe la Dunia kwa takribani miaka 4. --- Picha zote na mitandao ya kimataifa.
0 maoni:
Post a Comment