KUMBUKUMBU INAYO UMIZA LAKINI INAYO CHOCHEA MABADILIKO....
Tarehe kama ya leo 21.06. 2013 Ni kumbukumbu kwangu kwa kukamatwa na serikali ya ccm kupitia jeshi la polisi na kunifungulia mashitaka ya Ugaidi.
Sikukamatwa kwa kuwa niliitwa na kubambikizwa jina baya la ugaidi, sikukamatwa kwa kuwa nina roha mbaya ya kimiani kama walivyo taka kuitangazia dunia, hawakunikamata na kunitesa kwa kuwa mimi ni henry kilewo, hawakunikamata na kunisekwa gerezani kwa kuwa ni wapenda haki, hawakunikamata na kunidhalilisha kwa kuwa mimi ni mtoto wa maskini, bali walinikamata kwa kuwa mimi ni mwana chadema na chadema ni chama kinacho tishia uhai wao na tonge lao na udhalimu wao, wamenikamata ili kuitangazia dunia kuwa chadema ni chama cha kigaidi ili wapate mwanya wa kukichafua na hatimae kukifuta, ili wapumue, ili waahirishe mabadiliko ya lazima 2015.
Mke wangu alinipa moyo zaidi pale alipokuwa anaandamana kwani walidhani kuwakwangu ndani kungeweza kuidhoofisha Familia yangu kumbe walikuwa wanaijenga na kuiweka kuwa na utayari wa kupambana, vile vile mke wangu hakuandamana kwakuwa nimekamatwa bali kwakuwa alinyimwa haki ya msingi ya kuelezwa alipo mme wake na wakati huwo wanangu Lincon na Linston wakimuuliza Mama, Baba yupo wapi? Kama kuna watu walivunja haki za watoto walikuwa ni jeshi la polisi kwani walitaka kuwaharibu wanangu kisaikolojia kwa kutokutoa taarifa wapi alipo baba yao, Marafiki zangu wa karibu na wa mbali mmekua nanga iliyonituliza kwenye dhoruba.Chama changu kilikua Mwamba ulionisaidia kuhimili tetemeko na kadhia hizi zilizokera lakini zilizonijenga kiharakati-Shujaa Mpya kama kawaida alizaliwa.Nawashukuru watawala kwa kukisaidia chama changu katika kuzalisha shujaa mpya wa Mabadiliko.Mahasimu na hata Maadui asanteni sana.Ujumbe wenu niliupokea.Ujumbe wenu niliujibu kwa kustahimili yote lakini nilikataa kuwa mnyonge,nilikataa kuwasujudia na kuwapigia magoti badala ya kile ninachoamini na pia imani yangu iiliniongoza kumsujudia Muumba wangu pekee.Mahatma Gandhi alitufundisha kuwa watu hawa watatudharau,watatupuuza,watatucheka kisha wataanza kupambana nasi.Sitawahi kufanywa mnyonge kutokana na hila za maadui,watawala dhalimu na hata wasaliti wa harakati za mabadiliko.Nilitangaza Vita rasmi dhidi ya watu hawa nilipokubali kuingia gerezani.Vita hii haitakoma hadi ukombozi utakapopatikana.
Najua watu wengi waliumia juu ya jambo hili.
jambo ambalo wananchi wanapaswa kufahamu ni kwamba serikali zote dhaifu Duniani hutumia Dola ili kutisha wapambanaji na kuwarudisha nyuma kwakuwatia hofu kwa kutumia jela,mahakama,polisi, Usalama wa Taifa nk. Ukiweza kutokuwa na hofu na vikwazo hivi hakika utasimamia kile ukiaminicho hatakama utakutana na mateso makali basi mateso hayo yatageuka na kuwa dhabihu siku moja.
Ununda ambao nimeupata kupitia vitisho vya dola vimeweza kunijenga sasa na sioni jambo lingine la kuhofia tena hapa duniani kwa Wanadamu wenzangu, Zaidi ya kumkumbuka Steven Biko aliyewahi kunena ya kwamba, Ni heri kuishi miaka michache Duniani na jina lako libaki na kuishi kwa wema na haki milele, kuliko kuishi miaka mingi na siku ukifa jina lako likatoweka kama mzoga.
Vile vile maneno matakatifu kwenye vitabu yaliyotamkwa mara 366 yanazidi kunipa moyo wa ujasiri mkubwa sana kama neno"Usiogope" vile vile Mwanaharakati anayeheshimika Duniani ambaye alipatwa kuuwawa Mwaka 1968 Dr.Martin luther king Aliwahi kunena Nobody Can give you justice,Nobody Can give you Freedom or anything but u take it, Maneno hayo yote yananipa moyo sana yakuona ninawajibu wakuendeleza harakati za kudai mabadiliko bila woga wowote ule kupitia chama changu cha Chadema.
Kweli sinahofu tena ndani ya Nafsi yangu juu ya mtu yeyote yule anayepinga mabadiliko hata akiwa amesimama mbele yangu na mtutu wa risasi za moto nitasimama na kumpinga bila woga wowote ule ama hofu yeyote ile kwakuwa natambua wote tutaondoka na haki isipo patikana leo basi itapatikana kesho, naisipo patikana kesho basi itapatikana siku moja nisipo ishuhudia mimi HENRY KILEWO Vizazi vijavyo vitashuhudia na kusherekea kwa pamoja na kuimba Freedom now freedom now freedom now.. Sauti hizi zitapazwa kwa furaha itakayompendeza mungu na zenye baraka zake.
Kuishi kwa hofu ni utumwa, Kuishi kwa Hofu ni vita na kuishi kwa hofu ni dhambi "mtetezi wa wanyonge ambaye amepitia shuruba nyingi toka kwa watawala waliokataliwa, kijana Godbless Lema (Mbunge Arusha mjini)amekuwa akitukumbusha mara kwa mara kuwa katika mapambano ya kudai haki na usawa katika jamii, Ni heri ya vita inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu.
Dunia hii ya leo inateseka, Watu wanateseka siyo kwasababu ya vurungu dhuluma au maasi bali kwasababu ya ukimya wa Watu wema, yaani Watu wema wanapokaa kimya bila bila kukemea jambo ovu, Basi Maovu, Maasi hutamalaki.Ni heri kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti.
Nawatakia mapambano mema ya kudai haki na usawa wa mtanzania na kamwe sintorudi nyuma kudai mabadiliko kwenye Taifa langu.
WATATUUA KWA RISASI ZA MOTO WATAKUFA KWA PRESHA YA DHAMBI AHSANTENI NA MUNGU AWABARIKI.
HENRY KILEWO
Henry Kilewo akiwa na pingu katika gari ya Polisi chini ya ulinzi mkali siku alipokamatwa na Jeshi la Polisi. Ndio siku hii ambayo anasimulia historia mpya katika maisha yake. Katika kesi hiyo aliunganishwa na vijana wengine watatu na kudaiwa kumwagia tindikiali kijana mmoja wakati wa ucjaguzi mdogo wa Igunga Henry Kilewo katika moja ya shughuli zake kisiasa kupitia Chadema. Henry ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Kinondoni kwa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Mke wa Henry Kilewo ambaye pia ni mwanaharakati wa kutetea haki za watoto, wadada na wamama kupitia kipindi chake cha Wanawake Live kinachorushwa na EATV, Bi Joyce Kiria akiwa na mabango na watoto wake na mumewe akilalamikia Polisi kutojua muewe alipo wakati huo. Wakili Msomi Peter Kibatala akizungumza na waandishi wa habari kihusiana na utata wa kesi yenyewe kabla haijafutwa. Henry Kilewo, wa kwanza kulia akiwa Mahakamani Mjini Tabora na washitakiwa wenzake siku ya kufutiwa mashitaka ya ugaidi kifuatia shauri la pingamizi lililofunguliwa na Wakili Kibatala. Picha za Makataba, kwa hisani ya Tumaini Makene, Afisa Habari Chadema na Joyce Kiria
0 maoni:
Post a Comment