Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mataifa 31 Kushiriki Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba

MATAIFA 31 na kampuni zaidi ya 500
zimethibitisha kushiriki maonyesho ya
38 ya Kimataifa ya Dar es Salaam
(Sabasaba).
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade,
Jacqueline Maleko, alieleza hayo jijini
Dar es Salaam juzi katika hafla ya
kusaini mkataba wa udhamini wa
mawasiliano na Kampuni ya Vodacom.
“Maonyesho haya yamekuwa kiungo
kikubwa kati ya makampuni ya nje na
ya ndani, na pia yanatoa nafasi kwa
kampuni hizo kukutana na wateja wao
na kuzungumza ana kwa ana,”
alisema.
Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa
washiriki ambao hawajajiandikisha
kwa ajili ya mchakato wa kutafuta
washindi katika makundi mbalimbali
kuchukua fomu na kujiandikisha.
Pia aliwataka washiriki kujiandaa
kutembelea maonyesho hayo, ili
kupata fursa za masoko, uwekezaji na
ajira na kusema kuwa milango
itafunguliwa kuanzia Juni 28.
Mkuu wa Idara ya Masoko na
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,
Kelvin Twissa, alisema ushirikiano
kati yao na TanTarde umekuwa na
manufaa, kwani umewezesha kujenga
daraja na kutoa fursa kwa kampuni za
ndani na za nje.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO