KOMBE LA DUNIA 2014 NCHINI BRAZIL, Limekuwa si tu kombe la dunia la kusahau kabisa kuwazungumzia Uingereza dimbani kwa kusahau kama nao wanashiriki kombe hilo, bali pia limekuwa ni kombe ambalo hata baadhi ya makampuni yamepata ugumu kuweka picha sahihi za wachezaji wa timu hiyo ya taifa kwenye bidhaa za promosheni, kwani takwimu zinaonyesha wachezaji wa timu hiyo ya Uingereza hawajafanya lolote jipya ambalo lingeweza kuwafanya taswira zao kukaririka na kubakia vichwani mwa watu.
Kampuni moja lililojikita katika utengenezaji wa thamani za majumbani ambalo linategemea kuvuna fedha nyingi kwa kuuza vikombe vya kunywea chai na kahawa vyenye picha za wachezaji wa timu za mataifa mbalimbali yanayo shiriki Kombe la Dunia ikiwemo timu ya Taifa ya Uingereza, limejikuta kwenye mkumbo huo wa kutobaini utofauti wa picha ya mchezaji Chris Smalling na ile ya Rais wa Marekani Barack Obama. Imebainika kupitia Gazeti la Sunday Express.
Unaweza kununua bila utata vikombe vya wachezaji kama Steven Gerrard or Joe Hart or Wayne Rooney na wengineo lakini utata unakuja pale utakapo kuwa shabiki wa Chris Smalling na kuhitaji kikombe cha mchezaji huyo, utakutana na kitu cha utofauti na utastuka ukijiuliza maswali.. Jeh na huyu tena rais wa nchi nyingine ni mchezaji wa Uingereza?!!
Kikombe na utata:- Jina ni mchezaji husika timu ya taifa ya Uingereza, picha ni ya Rais wa Marekani Barack Obama.
Rais wa Marekani Barack Obama hachezi kama mtu wa kati kwa klabu ya Manchester United na wala timu ya taifa ya Uingereza.
0 maoni:
Post a Comment