Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

PPF Arusha Watoa Elimu ya Mifuko ya Hifadhi Kwa Wafanyakazi Sekta ya Ujenzi

Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini Bw Onesmo B Ruhasha na Afisa Muwezeshaji kutoka PPF Arusha, Bw Emmanuel Tarimo wameendesha semina kwa wafanyakazi wa sekta ya ujenzi Jijini Arusha na kukabidhi kadi za wanachama wapya 17 sambamba na kutoa fomu kwa wafanyakazi wengine kujiunga na mfuko wa pensheni.

Wawakilishi hao wa Mfuko wa Hifadhi wa PPF wametoa semina kwa wafanyakazi wa kampuni yakichina inayoitwa China Railway Jiangchang Engineering Co. Ltd wanaojenga jengo kubwa la PPF jirani na Hotel ya Kibo Palace Jijini Arusha.

Akizungumza na wafanyakazi hao, Bw Tarimo amewaeleza kuwa faida ya kuhifadhi fedha kwenye mifuko ya jamii ni manufaa ya baadae baada ya kustaafu au kupata ulemavu au kufariki. Kiwango cha kuchangia kwa kila mfanyakazi kitatokana na kiwango cha makubaliano cha mshahara baina ya mwajiri na mwajiriwa.

Mtaalamu huyo wa PPF ameeleza kuwa wajibu wa mwajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi ni wa kisheria na endapo atashindwa kufanya hivyo ataadhibiwa kisheria ikiwemo faini ya sh milioni 5. Sheria inasema uamuzi wa kuchagua mfuko wa kuweka fedha ni wa mwajiriwa mwenyewe na mwajiri anapaswa kuafiki chaguo la mwajiriwa wake.

PPF ni Mfuko wa Pensheni ulioanzishwa kwa sheria ya Pensheshi ya Mashirika ya Umma (Sura 372) chini ya kifungu cha 6(1) kwa madhumuni ya kutoa mafao ya uzeeni na mafao ya aina nyingine kwa wanachama wa mfuko huu. Mfuko wa PPF unaendesha uwekezaji kutumia michango ya wafanyakazi ili kuhakikisha thamani ya pesa inaendelea kuwepo. Mojawapo ya uwekezaji wa PPF Jijini Arusha ni jengo kubwa linaloendelea kujengwa lililobatizwa jina la PPF Plaza, likisimamiwa na Mshauri MD Consultancy Ltd na kujengwaa na hiyo kampuni ya kichina ya CRJE.

Kutoka kushoto; Injinia Norbert Nselu, Meneja wa Kanda ya Kasikazini Onesmo Ruhasha, Bw Chade na Afisa Mwezeshaji Emmanuel Tarimo wakimpongeza Chande, mfanyakazi wa CRJE upande wa umeme kwa kujiunga na mfuko wa PPF mara baadaya kumkabidhi kadi yake

Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini, Bw Onesmo B Ruhasha akitoa neno la ufunguzi katika smeimana kwa wafanyakazi wa ujenzi,  mradi wa jengo la PPF unaondelea barabara ya Old Moshi, Mtaa wa Engira.

Bw Ruhasha akizungumza na wafanyakazi hao wa CRJE kuhusu masuala mbalimbali ya mifuko y penshesni.

Akizungumzia mafao mbalimbali yatolewayo na mfuko wa PPF, Bw Tarimo amesema PPF wana Fao la Pensheni ya Uzeeni ambalo linalenga kumsaidia mchangiaji kuweza kuendelea na maisha ya siku zote baada ya kustaafu. Kushiriki pensheni hii lazima utimize vigezo hivi.

  1. Uwe umefikisha umri wa kustaafu
  2. Lazima uwe umechangia kuanzia miaka 10 au zaidi.

Mfuko wa PPF unafanya kazi kwa mujibu wa sheria ambayo inahitaji kila mfanyakazi kuchangia asilimia 20; ambapo mfanyakazi analazimika kuchangia asilimia 10 ya pato lake kwa mwezi na mwajiri anachangia kiasi kama hicho. Lakini pia inawezekana mwajiri akaamua kuchangia asilimia zaidi ya kumi na kiasi kinachobaki anaachiwa mfanyakazi.

Bw Tarimo alielezea pia uwepo wa Fao la Ugonjwa na kufafanua kwamba PPF wanatoa pensheni kwa matukio ya majanga yanayomsababishia mtu kushindwa kuendelea kufanya kazi kujizalishia. Vigezo vinavyozingatiwa kwa pesnhesni hii ni

  1. Ithibitike umepoteza uwezo wa kufanya kazi kama awali
  2. Uwe umetimiza miaka 10 ya uchangiaji mfuko.

Kwa ambaye hajafikisha miaka 10 atapewa kulingana na mchango wake na riba kiasi.

Fao jingine nilililoelezwa ni Fao la Kifo ambalo lina vitu vitatu vikuu; Utegemezi, Kifo na Elimu.

Kwa mtu aliyechangia mfuko kwa miaka 10 au zaidi, na kama ikitokea bahati mbaya amefariki mfuko utatoa pensheni ya kifo na fao la utegemzi na malipo mengine kwa miaka 3 ambayo ndugu watachukua.

Kwa mtu ambaye amechangia miaka kufikia 3, ikitokea amefariki mfuko utawalipia ada watoto wasiozidi wanne kulingana na uchangiaji wa marehemu hadi kidato cha sita.

Fao jingine ni Fao la Kujitoa
Ikitokea mwanachama amelazimika kukatisha mkataba kwa taratibu za mfuko, PPF itamrudishia michango yake. Lakini mfuko PPF wanashauri hata kama mfanyakazi atahama eneo moja ni vyema akaendelea na uhifadhi wake wa pesa huko aendapo badala ya kujitoa na kuanza upya

Afisa Muwezeshaji, Bw Emmanuel Tarimo akitoa maelezo ya namna mfuko wa PPF unavyofanya kazi wakati akiongea na wafanyakazi wa CRJE mapema leo asubuhi kwenye ofisi za ujenzi wa mradi huo.

Mshauri mkaazi wa mradi, Injinia N. Nselu akifuatilia mafunzokwwa umakini

Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini BW Ruhasha, Mwezeshaji Tarimo na Injinia Nselu wakisikiliza kwa makini maswali ya wafanyakazi hao hawaonekani pichani kabla ya kuyatolea ufafanuzi

Mwanachama  wa mfuko wa PPF akiuliza swali la namna gani mwajiri anapaswa kisheria kuwasilisha michango na kwa kiwango gani anastahili kumkata mfanyakazi wake.

Muwezeshaji Emmanuel Tarimo akifafanua jambo

Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini (mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara) akimkabidhi rasmi kadi ya uanachama wa mfuko wa PPF mwanachama mpya kutoka kampuni ya CRJE, Bi Stelah Zakaria

Mtaalamu wa umeme kutoka kampuni ya ujenzi ya CRJE, Bw Chande nae akipokea kadi yake ya uanachama kutoka kwa Menenja wa Kanda

Kijana mwingine ambaye naye alikabidhiwa kadi yake ya uanachama mbele ya halaiki.

Changamoto iliyoonekana katika semina hiyo ni watu wengi kutofahamu umuhimu wa kuwa sehemu ya mifuko ya hifadhi na halikadhalika ujanja ujanja wa baadhi ya waajiri kukwepa wajibu wa kuchangia asilimia 10 ya kile anachostahili kuchangia kwa mujibu wa sheria kwa kila mfanyakazi wake. Katika semina hiyo imefahamika kuwa waajiriwa wengi hupoteza haki yao toka kwa mwajiri kwa kutojiunga na mifuko ya hifadhi.

Akitoa neno la shukrani mwakilishi mkazi wa mradi wa jengo la PPF Plaza, Enjinia Norbert Nselu aliwashukuru PPF kwa kutembelea mradi na kutoa elimu kwa wafanyakazi hao na kuwaomba wasisite kutembelea tena kwa elimu zaidi.

Jumla ya wafanyakazi 42 walishiriki semina hiyo huku baadhi yao wakiwa tayari wanacham wa mfuko wa PPF na wengine wakiwa na uhitaji wa kujiunga na mfuko huo.

Aidha, wafanyakazi hao walipata fursa ya kuuliza maswali mblimbalia kutokana na changamaoto walizokumbana nazo ama kuhisi kuwepo kutokana na kujiunga na mfuko wa PPF ambapo wataalamu hao kutoka PPF waliwajibu kwa ufasaha.

Baadhi ya wafanyakazi waliohitaji kujiunga na mfuko huo wakipokea fomu za kujiunga rasmi kutoka kwa Mwenzeshaji Tarimo

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO