POLISI WA UFARANSA MATATANI KWA
UBAGUZI WA RANGI
Mzozo wa ubaguzi wa rangi unatokota nchini
Ufaransa baada ya picha kupatikana za
maafisa wa polisi wazungu wakiwa wamejipaka
rangi nyeusi huku wakiiga mienendo ya nyani
katika sherehe moja.
Mkuu wa polisi wa Ufaransa ameanzisha
uchunguzi juu ya suala hilo, baada ya picha
hizo kupatikana katika ukurasa wa Facebook
wa afisa mmoja wa polisi, imeripoti tovuti ya
Channel 4.
Maafisa hao wa polisi wanadhaniwa ni kutoka
kikosi cha Kremlin-Bicêtre, kusini mwa Paris.
Hii si mara ya kwanza kwa polisi wa Ufaransa
kutuhumiwa kwa ubaguzi wa rangi katika
mitandao ya kijamii. Mwaka 2013 afisa mmoja
wa kike wa polisi alitoa maoni ya kibaguzi
hadharani.
Shared from Salim Kikeke's facebook page
0 maoni:
Post a Comment