Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

News Updates: Mlipuko wa Bomu Zanzibar; Mtu Mmoja Afariki

Mtu mmoja ameripotiwa
kufariki huku wengine kadhaa
wakijeruhiwa katika shambulizi
la bomu kisiwani Zanzibar.

Baadhi ya waathiriwa walikuwa
wanaondoka katika msikiti
mmoja ulioko katika mji mkuu
wa Stone Town.

Haijulikani ni nani aliyetekeleza
shambulizi hilo ambalo linajiri
mkesha wa sherehe za kimataifa
za filamu katika kisiwa hicho.
Ni shambulizi la pili la bomu
mwaka huu.

Mnamo mwezi February,
mabomu mawili tofauti ya
kujitengezea yalilipuliwa nje ya
kanisa Anglikana mjini Stone
Town pamoja na mkahawa
uliokuwa karibu na kanisa hilo.
Kumekuwa na hali ya wasiwasi
wa kidini katika kisiwa hicho.

Source: BBC
http://t.co/JJpHRXq9ka

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO