Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Magdalena Sakaya (Mb) Ndiye Naibu Katibu Mkuu Mpya wa CUF Bara; Mtatiro Ammwagia Sifa Kemkem

Kufuatia kupitishwa kwa Mh Magdalena Sakaya kuchukua nafasi ya Julius Mtatiro kama Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Mtatiro ameandika ujumbe huu kama salamu za Pongezi kwa Sakaya kwa uteuzi huo. Hii hapa chini isome.

HONGERA MHE. MAGDALENA SAKAYA (MB).

Iam proud of you dada MagdalenaSakaya‬ (MB), NAIBU KATIBU MKUU MPYA, Chama Cha Wananchi CUF - Tanzania Bara.

Wewe pamoja na sekretariati mpya ya chama, nawatakia kila la heri katika majukumu ya kujenga chama chetu.

Nakuahidi wewe binafsi, viongozi na wanachama wetu wote ushirikiano mkubwa sana wakati wote ambapo mtakuwa mkipambana kukijenga chama.

Jambo moja ambalo ni muhimu, mimi naamini sana katika uwezo wa kina mama. Wewe umekuwa mbunge wetu muhimu sana na umeing'arisha CUF ndani na nje ya Bunge.

Natumai kuwa utatumia uzoefu wako mkubwa kukilinda na kukijenga chama katika nafasi ya NAIBU KATIBU MKUU BARA ambayo tumekukabidhi leo.

Nitumie fursa hii pia kuwashukuru viongozi wetu wakuu wa chama, Prof. Lipumba, Juma Duni Haji na Maalim Seif Hamad bila kumsahau Makamu Mwenyekiti mstaafu Mzee Machano Khamis Ali. Katika nyakati zote tulizofanya kazi pamoja nimejifunza mengi kutoka kwenu, nidhamu ya uongozi, uvumilivu, busara, hekima, mashirikiano na mengine mengi.

Miaka mitatu ambayo nimeongoza ofisi ya Naibu Katibu Mkuu Bara nimekuwa mkomavu sana, nimekuwa kiongozi imara na nimechota hekima, busara, uadilifu na nidhamu kutoka kwenu. Kupumzika majukumu haya makubwa ni faraja kwangu na kunanipa sasa muda wa kutosha wa kukamilisha shahada yangu ya tatu ya sheria.

Sitasita kuzidi kutumia uzoefu niliopata kuineza CUF na kuhakikisha inaweka mizizi Tanzania Bara. CUF ni kila kitu kwangu na bado najiona NINA DENI KUBWA katika chama changu, bado leo, kesho na kesho kutwa ntakuwa nafikiria NINI NIKIFANYIE CHAMA CHANGU na siyo CHAMA KINIFANYIE NINI.

Baraza Kuu lililochaguliwa hivi sasa lina uwezo mkubwa sana kuliko lililopita, hili lina wajumbe wengi vijana, wengi wanawake na wazee washauri wachache. Baraza hili litatuvusha vema chini ya uongozi wenu.

Nitazidi kuwa balozi wa chama changu usiku na mchana. Nimekuwa Mkurugenzi wa kitaifa wa chama nikiwa na miaka 26 na nimekuwa Naibu Katibu Mkuu nikiwa na miaka 28, ni nadra sana vijana kupata fursa kwa umri huo. Ni mara chache sana vijana wanaaminiwa kiasi hicho.

Naishukuru sana familia yangu, mke wangu Zakia Hassan na watoto wangu Faustina, Alexander, Elvis na Alma kwa kuwa wavumilivu wakati wote ambapo nilitingwa na majukumu ya kitaifa. Nawashukuru sana ndugu zangu wote ambao walinipa ushauri muda wote, marafiki na wote wenye mapenzi mema na kila aliyekuwa na mchango muhimu katika utendaji wangu.

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu Mstaafu,
Chama Cha Wananchi CUF,
Tanzania Bara.
28/06/2014.

Naibu Katibu Mkuu Mpya CUF Bara, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho Mkoa wa Tabora katika moja ya shughuli zake za kisiasa mkoani humo Naibu Katibu Mkuu wa zamani Julius Mtatiro Picha Zote na Kapipi Blog!
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO