Msafiri Mtemelwa (pichani) aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Kampeni na Uchaguzi CHADEMA, ameomba kuondoka rasmi kwenye chama hicho.
Habari ambazo zimetufikia kutoka kwa watu wake wa karibu zinasema kuwa Mtemelewa aliomba kukutana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, ili walau apate kitu chochote kutoka kwenye chama hicho kwa maana ya ‘mkono wa kwa heri’, kwa kuwa amekuwa mtumishi wa chama hicho kwa nafasi ya ofisa kwa muda mrefu (tangu alipojiunga na CHADEMA), hivyo afikiriwe katika hali yoyote.
Habari hizo zimezidi kutiririka zikimnukuu Mtemelwa akiwaambia watu wake wa karibu kuwa hakutegemea ushirikiano alioupata katika maombi yake ya kufikiriwa kupewa mkono wa kwa heri kwa kuzingatia nafasi yake aliyokuwa nayo ya Ofisa, ambayo inasemekana kwamba alikuwa na fikra hasi kuwa asingesikilizwa kutokana na matendo yake kwa nyakati tofauti tofauti dhidi ya chama hicho.
Kinyume na matarajio yake, Katibu Mkuu wa CHADEMA alimsikiliza Mtemelwa kuhusu maombi yake, ambapo muombaji alikubaliana na kiwango kilichopangwa kwa kuzingatia maombi yake, huku pia akipewa notice ya mwezi mmoja, kwa maana ya kwamba angelipwa ‘mkono wa kwa heri’ pamoja na stahili ya posho yake ya mwezi mmoja huu wa sita.
Sasa habari kutoka kwa marafiki wake wa karibu (ambao wanamfahamu kwa tabia ya uropokaji na kutotunza neon), wamemnukuu akianza kulalamika namna anavyoshawishiwa afanye mkutano na waandishi wa habari ili eti atangaze kuwa amehama ndani ya CHADEMA lakini anakidai chama hicho.
Maelekezo hayo anayapata kutoka kwa MM na MM 1 (hawa wanajulikana) na kundi lao ambao nao wanapata maelekezo kutoka kwa walioko nyuma yao wanaowapatia fedha za mkakati wa kupambana na CHADEMA.
Kutokana na tamaa ya fedha (ni moja ya sifa zake kama itakavyooneshwa hapo chini), Mtemelwa kasikika akiwaambia rafiki zake kuwa amekubali kufanya press conference kati ya leo Jumapili, Jumatatu ya kesho au keshokutwa Jumanne. Tayari MM 1 yuko anandaa taarifa kwa vyombo vya habari ambayo Msafiri Mtemelwa atatakiwa kuisoma mbele ya waandishi watakapoitwa!
Makubaliano ya kikao hicho ni kwamba ndani ya hiyo taarifa kwa vyombo vya habari, MM 1 atatakiwa kutengeneza kila aina ya uongo anaoweza kadri ya kipawa chake cha kupika mambo kinapoishia.
Wanasema kuwa uongo au matusi dhidi ya CHADEMA na viongozi wake yatakayosemwa na Mtemelwa yanaweza kuwarubuni watu wachache kwa sababu eti alikuwa Ofisa wa Chama hicho.
Mtemelwa amewahi kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Vijana wa NCCR-Mageuzi kabla ya kuhamia Chadema. Akiwa NCCR alishirikiana na Augustine Mrema kwenye ‘mission’ iliyotumika kukirudisha nyuma kama si kukiua chama hicho, akihusishwa na kikundi hatari maarufu kama Black Mambaz wakati huo. Wadadisi wa mambo wanadai huenda amejiona ni ‘misfit’ ndani ya CHADEMA na hivyo kuomba kuondoka ‘rasmi’ kwenye chama hicho.
Aidha taarifa zinaeleza zaidi kuwa maboresho yanayoendelea ndani ya CHADEMA ya kujipanga kwa ajili ya majukumu makubwa mbele ya safari, yamekuwa yakimnyima raha kwa sababu atalazimika kurudi kutumikia nafasi yake stahili yaani ya uofisa ambapo angepaswa kuwa chini ya moja ya kurugenzi za chama hicho.
Hiyo inatokana na kwamba chama hicho kimeondoa Kurugenzi ya Kampeni na Uchaguzi katika mfumo wake, kwa sababu kwa namna chama hicho kinavyoendesha shughuli zake na operesheni, wakati wa kampeni za uchaguzi, chama kizima huwa kinahusika, sasa majukumu mengine ya kurugenzi hiyo yakarudishwa chini ya ile Kurugenzi ya Benson Kigaila na machache yamekuwa chini ya Kurugenzi ya Uenezi.
Baada ya kujiona ni ‘misfit’ amefikia hatua ya kuomba aondoke, kuliko kuendelea na nafasi yake ya Ofisa wa Makao Makuu. Kwa mujibu wa vikao vya mamluki na wasaliti vinavyoendelea kufanyika, ameagizwa afanye hiyo press conference ya kutukana CHADEMA, kutukana viongozi na kuzua uongo mwingine, wakati wowote kuanzia sasa, kama alivyofanya akiwa NCCR, TLP, CUF na mara kadhaa alipokuwa hapo hapo CHADEMA.
0 maoni:
Post a Comment