Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

JUMA PINTO KUWA MGENI RASMI KATIKA BONANZA LA TASWA JUNI 28 ARUSHA

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo nchini
(TASWA), Juma Pinto, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika bonanza la
vyombo vya habari kanda ya kaskazini, June 28 mwaka huu ambalo
limedhaminiwa na kampuni ya hia nchini (tbl)
Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma akizungumza na waandishi wa
habari, palace hoteli katika kikao cha kutangaza zawadi na wadhamini
wa bonanza hilo.alisema maandalizi ya bonanza hilo  ambalo wadhami
wakuu ni kampuni ya bia nchini (TBL) yamekamilika.
Alisema Pinto ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya  hifadhi ya Mamlaka ya
Ngorongoro, anatajiwa kutoa zawadi kwa washindi, ambapo bingwa anavuna
kikombe na fedha taslimi 200, 000.
Mshindi wa pili katika soka atavuna 100,000, mshindi mpira wa pete
atavuna 100,000 huku timu yenye nidhamu itapokea tsh 50, 000.
Awali Mwenyekiti wa Taswa mkoa wa Arusha, Jamila Omar alisema timu za
wanahabari na wadau wa habari, watachuana katika soka, mpira ya pete,
kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mbio za magunia.

Aliwataja wadhamini wengine kuwa ni Mega trade, Mamlaka ya hifadhi
Ngorongoro, Kampuni ya Tanzanite forever,  TANAPA,Coca Cola, Pepsi
Arusha, Aicc,Alphatel na palace Hotel.
Timu ambazo zitashiriki ni Triple A, Sunrise radio, AJTC, Wazee Klabu,
Taswa Arusha, Radio 5, ,Arusha One, Mj radio, Radio ORS kutoka mkoa wa
Manyara na  NSSF.
Katika kikao hicho, ,Meneja masoko wa mega Trade alikabidhi the hundi
ya udhamini kiasi cha Tsh 1.5 milioni huku, Meneja matukio wa TBL
kanda kaskazini  Fred Sarakana akitangaza Tbl kuendelea kuwa wadhamini
wakuu wa bonanza hilo na kuwataka wanahabari kujitokeza kushiriki.

katibu wa Taswa Musa juma kulia akiwa anapokea cheki ya shilingi milioni moja laki tano kutoka kwa afisa masoko wa Kampuni ya Megatrade Godluck Kwayu

katibu wa taswa wa kwanza  kushoto  Musa juma akiwa
anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na bonanza la taswa
linalotarajiwa kufanyika jumamosi katika viwanja vya general trye
jijini hapa wa katikati ni meneja matukio wa TBL Chris Salakana akifuatiwa na mwenyekiti wa taswa Jamila Omary

  katibu wa chama cha waandishi wa habari  Mussa Juma
akiwa  na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo
Arusha (TASWA) Jamila Omary wakiwa wana pokea cheki ya  shilingi
milioni moja na laki tano  kutoka kwa meneja masoko wa Megatrade
Gudluck Kwayu katika ukumbi wa hoteli ya palace mkoani arusha

waandishi wa habari waliouzuria katika kikao cha waandishi wa
habari kilichokuwa kikizungumzia tamasha pamoja na makabidhiano ya
cheki

 

 

CHANZO: LIBENEKE LA KASKAZINI

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO