Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BBC - UK yakumbwa na uhaba wa mbegu za kiume

Uingereza inakabiliwa na upungufu wa Mbegu
za kiume hali ambayo huenda ikalazimu kiliniki
za matibabu ya uzazi nchini humo kuchukua
mbegu duni.
Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la
matibabu ya uzazi nchini humo BFS.
Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea
shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na
mahitaji yake nchini humo.
Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan
Pacey amesema kuwa ana wasiwasi kwamba
baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa
vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu
hizo.
Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na
mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha
iwapo mbegu duni zitatumiwa.
Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na
kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya
wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane
ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi
walipendelea kuficha majina yao.
Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi
kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya
uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta
watoto wao wenyewe.
Hatahivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za
kiume bado upo.
Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa
binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya
mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya
kigeni.
Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu
kumi mnamo mwaka 2005.

Picha: Mitandao
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO