Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Dr. JAKAYA KIKWETE NA MARAISI WASTAAFU WASHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU MHASHAMU AMEDEUS MSARIKIE MJINI MOSHI

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za Mwisho mbele ya jeneza la Askofu Mstaafu jimbo Katoliki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa misa ya Mazishi iliyofanyika katika kanisa na Kristu Mfalme, mjini Moshi juzi

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Askofu Mstaafu Jimbo katoliki la Moshi,Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi juzi

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Askofu Mstaafu jimbo Katoloki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjini Moshi juzi

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) akitoa heshima zake za mwisho kwa Askofu Mstaafu wa Kanisa Katoliki nchini, hayati Amedeus Peter Msarikie, katika misa ya kumuaga iliyofanyika jana katika Kanisa la Kristo Mfalme, Mjini Moshi.Picha na Freddy Maro-IKULU

---

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete juzi, Alhamisi, Februari 14, 2013 ameungana na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Moshi na kutoka sehemu nyingine nchini, kumzika Askofu Mstahivu (Bishop Emeritus) Amedeus Peter Msarikie.

Rais Kikwete aliwasili  kwenye Kanisa Kuu la Kristo Mfalme mjini Moshi kiasi cha saa sita na dakika tano mchana kuungana na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa na mamia kwa mamia wananchi kwa ajili ya mazishi ya Askofu Msarikie ambaye alifariki dunia Alhamisi iliyopita, Februari 7, 2013 kwa ugonjwa wa saratani katika hospitali moja mjini Nairobi, Kenya.

Mara baada ya kuwasili, Rais Kikwete alitia saini kwenye kitabu cha maombolezo na ikaanza ibada ya mazishi ilivyohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi wakiwamo maaskofu zaidi ya 20 kutoka majimbo mbali mbali ya Kanisa Katoliki nchini.

Mwili wa Marehemu Msarikie uliteremshwa kaburini kiasi cha saa saba na dakika 35 ndani ya Kanisa hilo na Rais Kikwete akaweka udogo kwenye kaburi na baadaye shada la maua.

Akizungumza kwenye mazishi hayo, Rais Kikwete amemwelezea Askofu Msarikie ambaye alikuwa Askofu wa Jimbo la Moshi kwa miaka 26 kama “kiongozi shupavu wa kiroho ambaye aliwalea vyema kondoo wa bwana. Lakini pia alikuwa kiongozi hodari  kwa maendeleo ya jamii yaliyowanufaisha waumini wake na hata wale wa madhehebu na dini nyingine.”

Amesisitiza Rais Kikwete: “Kwa kweli sote tumepoteza mtu muhimu. Tunamfahamu marehemu Baba Askofu Msarikie kwa mema mengi aliyowatendea watu wa jimbo lake, ya kiroho na ya maendeleo. Mimi binafsi, wana-moshi na Watanzania kwa ujumla tutamkumbuka na kumuenzi Baba Askofu Msarikie kwa mema mengi aliyowafanya wanadamu wenzake na nchi yetu.”

Taarifa kwa hisani ya Gadiola Emmanuel

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO