Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Hiace yaacha njia na kujeruhi 3 na kuua mmoja Jijini Arusha leo; Chanzo ni ushuru wa maegesho

DSCN7677Wananchi wa Jijini Arusha wakiangalia gari aina ya Totoya Hiace yenye namba za usajili T 173 BGS ambayo mmiliki wake hakuweza kufahamika mara moja, ikiinuliwa na winchi maalumu baada ya kuacha njia na kugonga watu wanne na kupelekea kifo cha mtu mmoja papo hapo mchana wa leo Jijini Arusha.

Kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda wa ajali hiyo, inaelezwa kuwa mara baada ya ajali hiyo dereva na mtu mwingine anaeelezwa kutoka kampuni ya ukusanyaji ushuru wa maegesho walikimbia. Kisa cha ajali hiyo kinahuisiwa kuwa ni msuguano baina ya watu hao wawili ndani ya gari.

Shuhuda mmoja amezungumza na Blogu hii na kueleza kwamba jumla ya watu wanne wamejeruhiwa na mmoja wao kupoteza maisha. Mtu aliyefariki anaelezwa kuwa ni mama mmoja wa jamii ya Kimasai aliyekuwa anapita pembezoni mwa barabara jirani na makutano ya Mtaa wa Wapare na Lindi akiwa na mwenzake ambae yeye amenusurika kifo.

Mtu mwingine ni ijana aliyetambulika kwa jina moja la Jumanne ambae ni muuza viatu maeneo ajali ilipotokea ambapo taarifa zinaeleza yeye amejeruhiwa mguuni.

DSCN7683

DSCN7680

DSCN7682

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO