Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira Kutoka Zanzibar: Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein Atoa Heshima za Mwisho kwa mwili wa Marehemu Padri Evarest Mushi na baadae kuongoza Mazishi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akitia saini kitabu cha maombolezi ya Padri Evarist Gabriel Mushi,katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar,ambapo alifika kutoa salamu ya mwisho kwa Padri huyo,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja,(kushoto)  Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akiwasalimia wananchi wakati alipofika katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar kutoa salamu ya Mwisho kwa Padri Evarist Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao wakati alipofika katika Kanisa la  Minaramiwili Mjini Zanzibar kutoa salamu ya Mwisho kwa Padri Evarist Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

 

Baadhi ya Waombolezaji wakiwa ndani ya Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar wakati wa kutoa salamu ya Mwisho kwa Padri Evarist Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akitoa salamu ya Mwisho kwa mwili wa Marehemu Padri Evarest Mushi,katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar, Padri Gabriel Mushi,aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikana Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja,(katikati) Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Antony Banzi,akiongoza  sala  wakati wa mazishi ya  Marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyekufa kwa kupigwa risasi Jumapili Iliyopita na kuzikwa leo katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya kaskazini B Unguja leo.

Askofu wa Kanisa  Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Vijana waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha jeneza lenye mwili wa marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,katika kaburi alilozikwa  leo katika viwanja vya kanisa la Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa.

Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akitia udongo  katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi Emanuel Nchimbi ,akitia udongo  katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja

Vijana waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha udongo wakati wa mazishi ya marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,katika kaburi alilozikwa  leo katika viwanja vya kanisa la Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa.

Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadham Policup Kadinari Pengo,kwa pamoja na maaskofu wengine wakichomeka Msalaba katika kaburi la marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukanwa

Picha na Ramadhan Othman Ikulu-Zanzibar

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO