Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

AZAM YAICHAPA AL-NASRI 3-1; MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Kiungo wa timu ya Azam FC, Bolou Kipre (kushoto) akitafuta mbinu za kumtoka mshambuliaji wa El-Nasir FC ya Sudan ya Kusini, Abdallmelik Sebit, wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Azam, imeibuka na ushindi wa mabao 3-1. Mabao ya Azam yamefungwa na Abdi Kassim, katika kipindi cha kwanza, na mabao 2 yamefungwa na Kipre Tchetche katika kipindi cha pili.

Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao la pili la timu yao lililofungwa na Kipre Tchetche (katikati) wakati ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya El -Nasir ya Sudan ya Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Kipre Tchetche (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Al-Nasri.

Jabir Aziz akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa El Nasir FC ya Sudan ya Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Azam FC, Brian Umomy akiwatoka walinzi wa timu ya El-Nasir FC ya Sudan ya Kusini, Jacob Osuru na Abdallmelik Sebit katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha el Nasir ya Sudan ya Kusini

Kikosi cha Azam FC

Mashabiki wa Azam, wakishangilia. Picha Zote na Dande JR

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO