Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Papa ahutubia baada ya kujiuzulu

 

Papa anatarajiwa kujiuzulu rasmi mwishoni mwa mwezi Februari

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Benedict wa kumi na sita amewashukuru waumini kwa maombi yao kwake katika hotuba yake ya kwanza hadharani tangu kutangaza kuwa anajiuzulu

Papa alishangiliwa na maelfu ya watu alipokuwa anajianda kutoa hotuba yake ya kila wiki mjini Vatican.

Alisema anajiuzulu kwa sababu anaelewa fika kuhusu hali yake ya kiafya inavyoendelea kudhoofika na anavyoishiwa na nguvu kutekeleza majiku yake.

Baadaye leo ataongoza misa yake ya mwisho katika kanisa ya St Peter's Basilica.

Tangazo la kujizulu alilitoa mwishoni mwa Februari,

Papa mwenye umri wa miaka 85, na ambaye jina lake kamili ni Kadinali Joseph Ratzinger ataendelea na majuku yake kama kawaida hadi siku atakapojiuzulu rasmi.

Katika muda wa wiki sita zijazo, Papa mpya anatarajiwa kuteuliwa.

Akiwa na umri wa miaka 78, kadinali Joseph Ratzinger, alikuwa mmoja wa Papa wazee zaidi kuwahi kuteuliwa kuongoza kanisa

Alichukua wadhifa wake wakati ambapo kanisa lilikuwa linakumbwa na kashfa nyingi ikiwemo visa vya kuwaharibu watoto vilivyofanywa na makasisi wa kanisa hilo

BBC Swahili

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO