Rais Barack Obama, akitoa hotuba ya hali ya kitaifa Feb. 12, 2013
Rais wa Marekani Barack Obama ametoa hotuba yake Jumanne usiku juu ya hali ya kitaifa. Mojawapo ya maswala aliyoyapa uzito yakiwa swala la uchumi na ajira. Akigusia moja ya mambo yenye utata Bw. Obama alitoa wito tena kuwe na juhudi madhubuti za kufanya mabadiliko katika sheria juu ya umilikaji wa silaha.
Alisema yale machache aliyozungumzia katika hotuba ya Jumanne usiku yatakuwa muhimu ikiwa mabaraza ya bunge yatakubaliana kulinda kile alichosema ni raslimali muhimu sana -nao ni watoto. Pia aliwataka wabunge kupigia kura mswada wa kuchunguza historian na tabia za watu wanaonunua bunduki na kuondoa silaha za kijeshi mitaani ili kulinda maisha ya raia wa Marekani wanaoendelea kuuawa kiholela na watu wenye bunduki .
Ghasia za bunduki zimekuwa suala kubwa tangu mauaji ya halaiki ya mwezi Desemba ya katika shule ya watoto ya Sandyhook jimbo la Connecticut .
Rais Obama aliahidi tena kuhakikisha nafasi sawa kwa wanajeshi wote ikiwa ni pamoja na mafao kwa familia zao hata kwa wale wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Amesema pia wanajeshi wa Marekani wataondoka Afghanistan kama ilivyopangwa mwaka wa 2014 na kwamba Marekani ni taifa lenye bora zaidi kuliko yote duniani.
Chanzo: Voice of America/Swahili
0 maoni:
Post a Comment