Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: KIKAO CHA NEC YA CCM, DODOMA LEO

Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa kuendelea na semina, leo kwenye Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO@Nkoromo Blog)

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa semina iliyoanza jana, na kuendelea leo kwenye ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Pamoja naye ni Dk. Sheni na Kinana

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji, kabla ya kuanza kikao hicho leo.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisahuriana jambo ukumbini na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, kabla ya kikao kuanza leo

Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete akimsalimia Katibu wa NEC Siasa ana Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro kabla ya kikao kuanza ukumbini. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye

Hali ndani ya ukumbi ilikuwa kama hivi kabla ya kikao kuanza. Kushoto Kabisa ni Nape na Zakia Meghji na juu-kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia wajumbe. Na Kulia chini ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhamed Seif Khatib na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakiteta jambo

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Vuai Ali Vuai kabla ya kikao kuanza

Wajumbe wa NEC  Profesa Anna Tibaijuka na Mzee Mtandika wakibadilishana mawazo ukumbini

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akichati jambona Mjumbe wa NEC, Samwel Sitta na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kikao

Nape (kulia) akichangia kwenye mazungumzo hayo kati yake na Dk. Asha-Rose na Sitta

Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, ambaye sasa ni Mjumbe wa NEC, William Mukama akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzake wa NEC Profesa Juma Kapuya ukumbini

Hii ndiyo Sekretarieti inayofuatilia na kuweka kumbukumbu ya mijadala inayozungumzwa kwenye mkutano huo

HII UNAONAJE?  Mjumbe wa NEC, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe akiteta jambo na Mzee Mtandika

Katibu Mkuu wa UWT, Sophia Simba akijadiliana jambo wa Wajumbe wenzake wa NEC ukumbini. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo Ana Makilagi.

Dk. Asha-Rose Migiro akishauriana jambo na Nape

TUKIFANYA HIVI MAMBO YATANYOOKA AU SIYO? Inaelekea ndivyo Dk. Asha-Rose Migiro alivyokuwa akisema kumwambia Nape katika mazungumzo yao ukumbi kabla ya kikao

HAPO VIPI? Katibu wa Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib anaonekana kumuuliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati wakibadilishana mawazo kabla ya kikao kuanza

SALAMU! Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa, Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia wajumbe wenzake wa NEC ukumbini kabla ya kikao kuanza

Wajumbe wakisubiri kwa hamu kikao kuanza

Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal (kulia) na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa safu ya mbele na baadhi ya wajumbe kwenye kikao hicho.

Baadhi ya wajumbe wakipitia nyaraka muhimu kabla ya kikao kuanza

Aliyekuwa Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma aka Mama Mshua (kulia) akimsalimia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabiba nje ya ukumbi. Katikati ni Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba

ENZI ZETU ZA IGUNGA VIPI? Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba anaonekana kumuuliza swali hilo Mjumbe wa NEC, aliyekuwa mbunge wa Igunga  Dk. Dalaly Kafumu walipokutana nje ya ukumbi kabla ya kikao kuanza

SHIKAMOO BOSI WANGU WA ZAMANI! Kaim Katibu wa CCM wa mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda akiwa na Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, William Mukama nje ya Ukumbi. Sixtus amewahi kuwa Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi kabla ya kuhamishiwa Morogoro mwaka jana wakati Mukama akiwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa.

CCM MAMBO SAFI TU! Mukama akimwambia Mjumbe wa NEC, Steven Wasira nje ya ukumbi

Wajumbe wa NEC wakiangua kicheko cha kutaniana kaba la kuingia ukumbini. Kutoka kulia ni Dk. Rafael Chegeni, Januari Makamba, Halimenshi Mayonga na Samwel Sitta

Wajumbe wakiwa tayari kuingia ukumbini kuanza kikao leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO