Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MKUTANO WA TATU WA WADAU WA SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII (NSSF)WAANZA LEO JIJINI ARUSHA

Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akizungumza na kuzindua wimbo maalum wa NSSF uliotungwa na Wasanii hapa nchini wajiitao All Stars,mbele ya wadau waliohudhuria mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.Kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akifafanua jambo kwa umakini  mbele ya  Wadau zaidi ya 1000 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike..

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akifafanua jambo mapema leo asubuhi wakati mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,ukiendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

Meneja wa kanda na anaeshughulikia Idara mbalimbali za serikali kutoka NSSF,Rehema Chuma akifafanua namna ya uendeshaji wa shirika hilo kwa  wadau waliohudhuria mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

Sehemu ya Meza kuu ya mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.

Pichani juu ni wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano

Pichani shoto ni Meneja Mahusiano wa PPF,Lulu Mengele na mdau mwingine wakifuatilia yanayojiri ndani ya mkutano huo unaoendelea hivi sasa.

Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini (CHADEMA),Mh Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akiwa sambamba na Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh Joshua Nasari (CHADEMA) na Wadau wengine wakifuatilia yanayojiri hivi sana kwenye mkutano wa NSSF.

Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya mkutano wa NSS unaoendelea hivi sana ndani ya ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha

Pichani shto ni Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mkoani  Njombe,Mh Deo Filikunjombe (CCM) akiwa na baadhi ya Wabunge Wenzake wanaohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ndani ya mkutano huo ambao umewakutanisha wadau zaidi ya 1000 kutoka sehemu mbalimbali jijini Arusha.

Mwenyekiti wa kikao cha awamu ya kwanza cha Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Bwa.Daudi Msangi akitoa utaratibu kwa Wanachama na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano huo unaoendelea ,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,kulia kwake ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza jambo na  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori mapema leo asubuhi kabla ya kuanza kwa mkutano wa shirika hilo.

Mmoja wa wajumbe wa NSSF,Peter Sumbi aliyekuwa akifanya kazi shirika la Wildlife Fund akitoa ushuhuda wake,namna alivyopata ajali na kufanikiwa kupata fao lake la ajali kazini kutoka kwa shirika la NSSF na hatimaye kufaidi matunda kupitia mfuko huo.

Pichani ni Mwenyekiti wa wasataafu wa TAZARA,Injinia Mwl.Sango akitoa ushuhuda wake kuhusiana na namna shirika la NSSF lilivyowasaidia wastaafu wa shirika la TAZARA,kupitia mfuko wa pensheni na fao la kujitoa.

Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd (wa tatu kulia)  na Mkewe,Mama Asha Seif Idd (wa pili kushoto) wakiwasili kwenye hoteli ya Mount Meru,Jijini Arusha usiku huu tayari kwa ufunguzi wa Mkutano huo utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.Wengine pichani ni Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (katikati),Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga (wa pili kulia),Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF,Ndg. Aboubakar Rajab (nyuma ya Waziri Kabaka) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (kulia).

Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akisoma hotuba yake usiku huu wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza machache usiku huu wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akipongezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF,Ndg. Aboubakar Rajab mara baada ya kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akitangaza majina ya washindi wa tuzo mbali mbali za NSSF kutoka mashirika,makampuni pamoja na watu binafsi.

Baadhi ya Washindi wa Tuzo mbali mbali za NSSF wakipokea tuzo zao hizo kutoka kwa Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd

Wakurugenzi Wakuu wa Zamani wakiwa na tuzo zao baada ya kupokea.

Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akiagana na Mke wa Makamu wa pili wa Zanzibar,Mama Asha Seif Idd.

Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira,Ndg. Eric Shitindi (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF,Ndg. Aboubakar Rajab.

Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio (kulia) akimtambuliza Meneja Mawasiliano wa PPF,Lulu Mengele kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe.

Zawadi kwa Mgeni Rasmi.

Zawadi kwa Mh. Waziri Kabaka.

King Kikii na Wazee Sugu.

Kigoma All Stars wakitigita stejini.

Mambo ya Kitamaa cheupee....

 

Wafanyakazi wa NSSF.

Wakurugenzi Wakuu wastaafu.

Wajumbe wa Bodi ya NSSF.

Waheshimiwa wabunge.

Wahariri wa vyombi vya habari hapa nchini.

Mambo yamenoga.

Picha ya pamoja na Baadhi ya Wakurugenzi wa Mifuko mbali mbali.

Picha ya pamoja na wakurugenzi wastaafu.

Picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya NSSF.

Picha ya pamoja na Wabumbe.

Picha ya pamoja na Washindi wa tuzo mbali mbali.

picha kwa hisani ya Woinde Shizza

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO