Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAJIMBO CHADEMA: UZINDUZI WA KANDA YA KASKAZINI, MBOWE AITAKA SERIKALI NA CCM IJIBU MAPIGO YA MAUJI YA VIONGOZI WA DINI GEITA NA ZANZIBAR

photo(10)

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mh Freeman Mbowe akiwa anaongea  na viongozi wa chama hicho leo (jana) jijini Arusha kutoka Kanda ya Kaskazni ni,Arusha,Manyara,Kilimanjaro,Tanga katika mkutano wakujadili sera ya majimbo

photo(12)

DSCF7692

Viongozi wa chama hicho ambao ni wajumbe wa mkutano huo

DSCF7693

DSCF7695

DSCF7697

DSCF7696

DSCF7703

DSCF7702

DSCF7701

KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida mwenyekiti wa chama cha demokrasia na
maendeleo(CHADEMA),Freeman Mbowe amesema kuwa mauji ya Viongozi wa
dini ambayo yametokea,katika mkoa wa Geita, na Zanzibar ni matokeo ya
CCM,na hivyo kama wataandelea kuendesha nchi kwa msingi hiyo bado nchi
itakabiliwa na mauji makubwa sana

Mbowe aliyasema hayo mapema leo wakati akiongea na wajumbe wa mkutano kutoka  kanda ya kaskazini iliyolenga kujadili sera ya majimbo ambayo itaweza kuhudumia mikoa ya kanda ya kaskazini katika shughuli za kichama na za kijamii

Alisema kuwa hapo awali Chadema kilishasema kuwa CCM isipuuzie
matatizo ya ubaguazi wa dini lakini chama hicho hakikusikia na badala
yake kiliendelea kujiendesha kwa misingi ya kubaguana kidini hali
ambayo sasa inanyima watu uhuru wa kuabudu na kufanya mambo yao

Alisistiza kuwa kama CCM  bado iliendelea kufanya ubaguzo wa dini kwa
misingi kuwa inakomoa Chadema lakini hawakujua na kutambua kuwa hali
hiyo inafanya mauaji ya kila siku ambayo sasa yameanza Geita lakini
Leo yameelekea Zanzibar mara baada ya Padri kuuliwa wakati akielekea
Kanisani kusalisha misa

“Leo kila mahali unasikia mauji ya dini lakini mimi nilishawaambia CCM
kuwa hiii sio hali ya kuendelea kuangalia lakini walujua  kuwa ni
siasa na wao  walifanya hivi kwa malengo ya kuwa wanatukomoa sisi
Chadema kwa kugawa Taifa katika Imani ya kidini sasa wamelikoriga
wanatakiwa kulinywa’aliongeza Mbowe

Katika hatua Nyingine Mbowe alisema kuwa wao kama Chadema wanalaani
Mauji ambayo yanatokea kila siku ndani ya Tanzania na kwa hali hiyo
hawataweza kuwagawa wananchi  katika misingi ya kidini kwa kuwa wote
wapo sawa na kama Nchi itaendeshwa hivyo ni wazi kuwa damu ambazo
hazina hatia zitamwagika kila mara.

“Chadema tunaalani kwa kweli haya mauji na kwetu Muislamu, Mkristo
wote ni wa moja na kamwe kiongozi ambaye ataonesha ubaguzi dhidi ya
wakristo na waislamu ni wazi kuwa tutamkimbia hatuwezi kuingiza
jitiada za CCM ndani ya chama chetu,na kuweka utaratibu wa kumwaga
damu ambazo hazina hatia kabisa’aliongeza Mbowe

Akiongelea suala la kanda ya kaskazini ndani ya chama hicho alisema
kuwa hiyo ni moja ya mikakati ambayo imewekwa na mbali na hilo pia
kupitia viongozi wa kanda ya kaskazini wataweza kujiwekea nafasi nzuri
sana ya kuchukua Nchi ya Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2015 hivyo
kufanya Nchi iwe huru zaidi kuliko  ilivyo kwa sasa

Mbowe aliongeza kuwa kanda ya kaskazini pia itaweza kuwa chachu ya
Maendeleo kwa kuwa itaweza kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo
zinawakabili kwa kuwa sasa kazi za maendeleo zitafanywa chini ya mikoa
minnne tofauti na hapo awali ambapo kila mkoa ulikuwa unajitegemea kwa
shuguli za kichama na za kichama

Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema katikati akiwa katika Uzinduzi wa Chadema Kanda ya Kaskazini.

Katibu wa Chadema Arusha Mh Amani Golugwa akiongea katika uzinduzi wa Chadema Kanda ya Kaskazini.

Kamanda James Ole Millya aliye katikati akiwa katika uzinduzi wa Chadema Kanda ya Kaskazini.

Muasisi wa Chadema Mzee Edwini Mtei Akiwa katika uzinduzi wa Chadema Kanda ya Kaskazini.

Mbunge wa Viti maalum Mh Lucy Owenya akiwa katika Uzinduzi wa Chadema Kanda ya Kaskazini.

Picha: Pamela Mollel na Chadema Blog!!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO