Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe akihutubia wananchi waliojitokeza katika mkutano mkubwa wa Chama hicho uliofanyika Jijini Arusha jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro katika Uzinduzi rasmi wa Kanda ya Kaskazini ya kiutawala kwa chama hicho, Kanda inayounganisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na na Manyara.
Mh Mbowe akihutubia.. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na wabunge wote wa Chadema kutoka mikoa tajwa pamoja na viongozi wote na madiwani wa Chadema kutoka mikoa hiyo.
Baadhi wa Kina Mama Wabunge wa Chadema na Viongozi wakifuatilia hotuba katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mhe Rose Kamili, Mh Cecilia Pareso, Mh Grace Kihwelu na Mh Cecilia Ndosi.
Dua/Sala kabla ya kuanza Mkutano
Mzee Fundikira mwenye umri wa miaka 95 akihutubia mkutanoni hapo.. Mzee huyu anasema alikuwa kwenye siasa tangu enzi za TANU lakini sasa yuko Chadema na kuwasihi wazee wenzake kutosita kujiunga na chama hicho.
Mbunge wa Rombo Mh Joseph Selasini
Mh Rose Kamili akisalimia wananchi
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akifafanua jambo mkutanoni hapo
Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Mh Israel Natse, Mbunge wa Karatu akihutubia
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwajibika. Mwanahabari wa Jamii Blog ya Jijini Arusha, Pamella Mollel akiwa miongoni mwao
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari nae alipata wasaa wa kuzungumza ambapo alieleza namna wanavyopata ukinzani Bungeni na jinsi walivyojipanga kukabiliana na hali hiyo.
Katibu wa Muda wa Kanda ya Kaskazini ambae pia ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Mh Amani Golugwa akifuatilia hotiba
Mzee Fundikira na baadhi ya madiwani wa Chadema
Mdau wa Blog hii , Imma Munisi (mwenye shati jeusi) akiwa miongoni mwa waalikwa na makamanda wengine wa Chadema, Chris na Kamnde.
Sehemu yalikopaki magari ya waheshimiwa wabunge na viongozi wa Chadema
Bosi wa Blogu hii (katikati) akipiga stori na wanachadema mara baada ya mkutano kuisha
0 maoni:
Post a Comment