Askofu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania dayosisi ya kaskazini kati Askofu Thomas lazier amefariki Dunia jioni ya jana Alhamis 7 Februari 2013.
Habari ambazo zimethibitishwa na katibu Mkuu wa dayosisi hiyo Israel Ole Karyongi zimesema kuwa askofu alikumbwa na mauiti majira ya saa 12 za jioni ya jana.
“Ni kweli baba Askofu amepita na tuko katika hali ya dharura ngumu na tungependa mtuachie nafasi ili tuwape taarifa juu ya msiba huu kesho”alisema Karyongi akizungumza kwa njia ya simu .
Askofu lazier ndiye askofu wa kwanza wa na mwanzilishi wa dayosisi hiyo ambayo awali ilikuwa ikiitwa dayossi Mkoani Arusha kabla ya mwaka juzi kubalishw ajina na kuitwa dayosisi ya kaskazini kati.
Ni msiba mkubwa mno katika Mkoa wa Arusha kutokana na askofu huyo kupata umaarufu katika kazi zake za kiroho na kijamii husasan jamii ya kabila la wamasai.
Anatajwa kushiriki katika kuendeleza jamii hiyo kielimu kwa kubuni na kuanzisha shule zaidi ya ishirini za sekondari zikiwemo maalum kwa ajili ya watoto wa kike.
Habari zaidi na CHARLES NGEREZA
Pichani: Askofu Thomas Leizer, katika siku za mwisho za uhai wake, akiwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya Selian Hospital Arusha Centre. Pamoja naye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe. Picha hii ilipigwa Tarehe 3 Februari 2013, ambapo viongozi wa CHADEMA [Mbowe na Lema] walifika kumjulia hali, baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazwa.
0 maoni:
Post a Comment