Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA NA HABARI: SIKU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA SHULE YA ARUSHA SEKONDARI YA JIJINI ARUSHA

DSCF7796

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mh.Godbless Lema pamoja na madiwani,walimu,wadau wa elimu,viongozi mbalimbali na wanafunzi wakiwa katika maandamano yaliyoanzia katika Halmashauri ya jiji la Arusha kuelekea katika shule ya Arusha Sekondari 23/2/2013 yaliyoanza mida ya saa mbili asubuhi ikiwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya shule hiyo

DSCF7881Mbunge wa Arusha  mjini Mh. Godbless Lema ameitaka serikali iboreshe maisha ya walimu ili kunusuru elimu nchini kufuatia hali mbaya iliyojitokeza katika matokeo ya kidato cha nne mwaka huu.

Lema amesema kuwa walimu wasipotizamwa maisha yao hali itazidi kuwa mbaya kwani wengi wanakwenda darasani mioyo yao ikiwa imepondeka nyumbani wameacha maisha magumu  hivyo wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa moyo.

“Hata tukiwatia moyo kiasi gani walimu bila kuboresha maisha yao ni kazi bure.Matokeo  ya kidato cha nne mwaka huu ni  mgomo tosha wa walimu sote tunaona yamekuwa janga kwa taifa” Alisema Godbless Lema

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shule ya Arusha sekondari iliyoko mjini hapa mnamo mwaka 1963,Lema ameitaka serikali ijikite katika kuboresha elimu na maslahi ya walimu ili kulinusuru taifa na adui ujinga na umasikini pamoja na ongezeko kubwa la wasiokuwa na ajira ambao huenda sambamba na ongezeko la watu ambao ni tegemezi

Mbunge huyo amewaasa wanafunzi kuacha tabia ya kuiga mambo ambayo si ya msingi na kuongeza kuwa wazazi wa siku hizi wanaonya kidogo kwani mara nyingi wanakuwa na msongo wa mawazo kutokana na ugumu wa maisha hivyo hawana muda wa kutosha wa kuwaonya watoto matokeo yake watoto wanakuwa na maisha magumu baadaye kutokana na misingi mibovu.

Vile vile mbunge huyo ameahidi kushirikiana kikamilifu na uongozi wa shule hiyo katika kusaidia kupata viwanja vya wazi  vya shule hiyo ambavyo vilichukuliwa kinyamela na watu wamejimilikisha kwani shule hiyo bado ina uhitaji wa maeneo zaidi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa,mabweni na nyumba za walimu.

Joseph Malamsha ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Arusha Sekondari amesema kuwa changamoto kubwa  inayowakabili ni ukosefu wa Maktaba ya kujisomea jambo ambalo linawapelekea wanafunzi kuzurura maeneo ya mjini pindi wanapomaliza vipindi vya darasani ama kusubiria kuingia shift,Tayari wamekwisha changisha milioni 35 kwa ajili ya ujenzi wa makataba ya kisasa ambayo itagharimu kiasi cha shilingi milioni 400 na hivyo amewataka wadau kujitokeza kuchangia ujenzi huo ili kusaidia kuinua elimu shuleni hapo.

“changamoto nyingine inayoikabili shule hii ni uchakavu wa mjengo hivyo amewaomba wadau wa elimu kuwasaidia kufanya ukarabati wa majengo ili shule hiyo iendane ongezeko la idadi ya wanafunzi ambao kwa sasa jumla yao ni wanafunzi 2000” Joseph Malamsha

Wakizungumza baada ya kumalizika kwa Maadhimisho hayo Hoyce Temu na Lawrence Mafuru  ambao ni watu waliosoma katika shule hiyo miaka iliyopita wanaeleza kuwa ni vyema serikali ikalitazama kwa undani suala la matokeo ya kidato cha nne ,na kuelezea kusikitishwa na asilimia 60% ya wanafunzi kote nchini waliopata division 4 na zero na kusisitiza kuwa hilo ni janga kwa wazazi,walimu ,jamii na taifa kwa ujumla.Hivyo hatua madhubuti zichukuliwe kuinusuru elimu yetu

DSCF7801

Wanafunzi wakionekana na nyuso za furaha huku huku mmoja wao akiwa amebeba bango lenye kuonyesha miaka 50 ya shule ya Arusha Sekondari

DSCF7911

Aliyekuwa Mkurugenzi wa benki ya NBC Lawrence  Mafuru ambaye alishawahi soma katika shule hiyo siku za nyuma toka mwaka 1987-1990 akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya shughuli hiyo kukamilika huku akieleza furaha yake ya kushiriki katika maadhimisho hayo

DSCF7807

DSCF7808

Hapa wanafuzi wa somo la upishi wakiwa wanaonyesha bites pamoja na juice kwa Wageni walifika katika jiko la shule

DSCF7811

DSCF7812

Hapa ikiwa muda wa kuonja mahanjumati,,kila mtu na kipande chake,,ahahahah

DSCF7822

Wanafunzi wakiwa wanaonyesha umahiri wao wa kuzungumza lugha ya Kingereza na Kifaransa kwa Mh,Mbunge pamoja na wageni waliofika shule hapo

DSCF7826

DSCF7827

DSCF7832

Katibu Mkoa wa Arusha wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Aamani Golugwa ambaye naye alishawahi soma katika shule hiyo akiangalia ramani ya jengo la shule

DSCF7834

DSCF7836

DSCF7838

DSCF7844

Mmiliki wa blogu ya  jamiiblog Pamela Mollel akiwa na wanahabari wa kituo cha Triple” A” Amiri Mongi katika maadhimisho hayo

DSCF7850

Kushoto ni Hoyce Temu aliyekuwa Miss Tanzania aliyewahi kusoma katika shule hiyo

DSCF7858

Kikundi cha sanaa cha maigizo kikifanya igizo lililokuwa likisisitiza wazazi,jamii kushirikiana na walimu katika maendeleo ya mwanafunzi na siyo jukumu hilo kuachiwa waalimu peke yao

DSCF7861

DSCF7867

DSCF7868

DSCF7900

Amani Golugwa akiwa na uso wa furaha baada ya ya kupokea cheti chake kama mwanafunzi aliyewahi soma katika shule hiyo (PICHA ZOTE NA STORI: JAMII BLOG YA JIJINI ARUSHA)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO