Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BUNGE KUSITISHA KURUSHA VIKAO VYAKE LIVE

BUNGE linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwamoja kupitia televisheni kwa madai ya kukomesha vitendo vya baadhi ya wabunge kukiuka kanuni za bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila kujua kwamba tabia hiyo inaleta picha mbaya katika jamii.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashilila jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge.

Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wanashindwa kufuata kanuni za bunge na kutumia nafasi hiyo kwa kutafuta umaarufu kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.

Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni za bunge makusudi na kusababisha kuleta vurugu bungeni wakati jamii ikiendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi.

Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.

Hivi karibuni baadhi ya kamati ikiwemo ile ya Mashirika ya umma POAC zimefutwa na kuacha maswali mengi kwa baadhi ya wananchi juu ya hatua hiyo.

Chanzo: Star Tv

Taswira: Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila Akizungumza na Waandishi wa Habari na Kuelezea umuhimu wa wabunge kuzisoma na kuzitumia ipasavyo kanuni za bunge ili kuondoa manug'uniko

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila akitoa somo kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa wabunge kuzisoma na kuzitumia ipasavyo  kanuni za bunge ili kuondoa manug'uniko yanayojitokeza pindi wanapozuiliwa na spika kuchangia mijadala au kutoa hoja bungeni kwa sababu ya kukiuka kanuni na umuhimu wa waandishi wa habari  kuzitumia taarifa rasmi za bunge katika utoaji wa taarifa zao.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila akitoa ufafanuzi kwa  waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa kanuni za bunge uliofanywa na baadhi ya wabunge wakati wa mkutano wa 10 wa bunge uliomalizika mjini Dodoma na mabadiliko yaliyofanyika kwa baadhi ya kamati kuondolewa  pamoja na uundwaji wa kamati mpya 3 zitakazoshughulikia Ushirikiano wa Afrika, Mashariki, Bajeti na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.Picha na Aaron Msigwa-MAELEZO

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO