Viongozi waliokuwa wakiendesha mdahalo huo wakiwa meza kuu.
Dr. Kitila Mkumbo akichangia mdahalo huo.Mmoja wa wananchi akichangia majadiliano hayo.
Wananchi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliohudhuria mdahalo huo.
JUMUIYA ya wanataaluma wa Chuko Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana walifanya mkutano kuhusu athari za sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya mtandaoni za mwaka 2015 ili kupata maoni mbalimbali juu ya sheria ya uhuru wa vyombo vya habari.
Mdahalo huo uliofanyika ukumbi wa Nkrumah wengi wao walichangia juu ya maboresho ya mswada wa sheria hiyo iliyojadiliwa bungeni kwamba iwapo Rais Kikwete atasaini sheria hiyo, ni dhahiri itawanyima uhuru na haki za msingi wanahabari na asasi za raia katika kutoa mchango wake wa utoaji maoni.
Walimtaka rais asisaini miswada hiyo kuwa sheria.
(PICHA/STORI:DENIS MTIMA/GPL)
0 maoni:
Post a Comment