Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Serikali na Mbunge Nassari Wapinga Hukumu ya Miaka 75 Kwa Watendaji wa Vijiji Arumeru

joshLile sakata la kufungwa miaka 15 kila mmoja kwa viongozi wanne wanne wa Serikali ya Kijiji cha Msitu wa Mbogo kilichopo Wilayani Arumeru  Mkoani Arusha limechukua sura mpya baada ya Serikali na Mbunge wa Jimbo hilo Mh Joshua Nassari kupinga hukumu hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Hasna Mwilima alisema kuwa Serikali inaheshimu misingi ya Sheria na utawala bora lakini kutokana na mazingira ya kesi hiyo ni muhimu kukata rufaa

Naye Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari amesema mbali na kuwaomba wanasheria wa Halmashauri kukata rufaa, naye ataongezea mawakili katika rufaa hiyo

“Ingawa mwenyekiti huyu ni wa CCM na wenzake, binafsi naamini kesi hii inatokana na mgogoro wa shamba la Tanzania Plantation na tunaipinga hukumu hii” alikaririwa Nassari akisisitiza zaidi.

Awali, viongozi hao, wote kupitia CCM wakiwa ni Mwenyekiti Ernest Samson na wajumbe wa Serikali ya Kijiji Julius Nyungusi, Saimon Samson, Edwin Deo na Juma Maulid walikuwa wanawatetea baadhi ya wananchi ambao walikuwa wamepewa sehemu ya shamba la Tanzania Plantation lenya mgogoro baina ya wanakijiji na mwekezaji wa Kihindi Pradeep Lodhia, na kuishia kutiwa hatiani na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo David Mwita kwa kosa la kupora fedha kwa mlinzi wa shamba Bw Petro Damas.

Katika kuonesha kuwa Nassari amedhamiria kuwapigania watu wake na maisha yao, ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Facebook kuwa..

“Mwl Nyerere aliwahi kusema , ukianza kula Nyama ya binadamu hutaweza kuacha, unaweza kujikuta unakula hata watoto wako mwenyewe.
Walizoea kutufungulia kesi za kughushi wanasiasa wa upinzani. Sasa wamepitiliza wamejikuta wakiwafunga hadi wanasiasa wanaotokana na ccm pale wanapojipambanua kuisimamia kweli.

Hata hivyo, Kama Mbunge sitakubali Mwananchi wangu yeyote awe wa CHADEMA ama wa CCM aonewe eti tu kwa sababu ya kushiriki kuipigania Haki.

Shamba la Karangai Sugar maarufu Kama Tanzania plantation lazima lirudi kwenye mikono ya wananchi kwani lilishafutiwa hati na Rais Mkapa mwaka 1999 mwezi December na barua kutoka wizara ya ardhi zenye maelekezo hayo zipo ma mimi binafsi ninazo.
Kwa nini hadi leo anayejiita muwekezaji raia wa Uingereza mwenye asili ya kihindi aendelee kuhodhi, kuuza na kukodisha ardhi asiyoimiliki kihalali???

Hivi kati ya Rais na muwekezaji nani mwenye Mamlaka juu ya ardhi ya Tanzania??
Tunajua Namna ambavyo fedha nyingi imetumika kumbambikizia kesi na hatimaye kumfunga mwenyekiti wa kijiji cha Msitu wa mbogo, kata ya mbuguni - Arumeru Ndugu Ernest. Na sababu ya Msingi hapa ni kukandamiza harakati za kuendelea kuidai ardhi hii yenye zaidi ya ekari elfu tatu (3000).
Nilikwenda Magereza siku ya jumapili kumwona na kumtia Moyo, lakini pia kumjulisha kuwa hatuliachi lipite.

Kwa kifupi ni kwamba, hatutarudi nyuma.”



Historia ya mgogoro
Arumeru Mashariki ni moja ya maeneo mengi nchini ambako kumekuwa na migogoro mikubwa ya ardhi.

Shamba hili limekuwa likivamiwa mara kwa mara na wakazi wa vijiji vya Msitu wa Mbogo na Karanga katika kuishinikiza Serikali kuligawa shamba hilo wanalodai kuwa lao na kwamba hati ya umiliki kwa mwekezaji ilishatenguliwa na Rais tangu mwaka 1999.

Mwaka jana wakazi wa Msitu wa Mbogo walituhumiwa kuvamia shamba hilo na kumjeruhi mlinzi Hamis Michael (25) ambaye alilazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Meru, Tengeru.
Mlinzi mwingine, Saigurun Mollel akaeleza kuwa kundi kubwa la wananchi hao walivamia shamba hilo na kung’oa mazao yaliyokuwamo.

Mgogoro huo ulimlazimu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh Magesa Mulongo kuingilia kati mwezi Machi mwaka jana na kuagiza usitishwaji wa shughuli zote katika shamba hilo hadi pale mgogoro huo utakapomalizwa na Serikali.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO