Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

VIJANA WA CCM WAJIPANGA KURUDISHA JIMBO LA ARUSHA MJINI KUTOKA KWA CHADEMA

uvccm

Wanachama na mashabiki wa chama cha Mapinduzi wametakiwa kujipanga kuhakikisha jimbo linarudi mikononi mwao kutoka kwa wapangaji ambao kodi yao imeisha chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kwenye uchaguzi ujao ocktoba mwaka huu na kuwa ushindi ni lazima kwa chama chao.

Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa vijana mkoani hapa Philemon Mollel wakati wakitoa neno la shukrani kwenye chakula alichowaandalia wanachama na mashabiki wa CCM pamoja na wananchi wa kata ya Unga ltd kwa ushindi walioupata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mollel aliwataka kuanza kujiandaa kuchukua jimbo hilo lililopo mikononi mwa Chadema kwani ushindi wa chama hicho upo wazi na kuacha migawanyiko isiyo na lazima ambayo iliwafanya kulikodisha jimbo hilo kwa mbunge wa sasa Godbless Lema.

Alisema kuwa migogoro iliyokuwepo ndani ya chama hicho hapo kabla iliwafanya kutoa mwanya kwa washindani kushinda na hivyo muda umefika wa kodi yao imemalizika sasa ni zamu ya chama hicho kurudisha jimbo hilo.

“Hakika natambua kuwa kila ukipanda mbegu nzuri utavuna mazao mazuri hivyo sisi tuliwapangisha hatukuwajua walahatukutaka kuwajua vizuri sasa tumevuna tulichakipanda kwa miaka mitano tusije tukajaribu tena kula sumu”alisema Mollel

Nae Diwani wa kata ya Unga Ltd Issa Said Aliwataka wakazi wa kata hiyo wakati ukifika wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kujitokeza kujiandikisha na baadae kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura ya maoni na kuwachagua viongozi.

Alisema kuwa kumekuwepo na wananchi wanaoshindwa kuitumia nafasi yao ya kikatiba kuwachagua viongozi na baadae wamekuwa wakitoa lawama kuwa wamechaguliwa viongozi wasiofaa hivyo akawataka kujitokeza kumchagua kiongozi wanaemtaka kwa manufaa ya kata yao na jimbo la Arusha na Tanzania kwa ujumla

“Kwanza namshukuru muumba na pili namshukuru Kamanda kwa kutimiza ahadi aliyoweka wakati wa kampeni kuwa atatoa Ng’ombe kwa kata itakayoshinda mitaa mingi na sisi kuibuka kidedea kwa kushinda mitaa mitano kati ya sita iliyopo kwenye kata hii”alisema Said

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Unga Ltd Sophia Munisi alisema kuwa watahakikisha chama hicho kinapata ushindi katika uchaguzi uliopo mbele yao tena wa kishindo kuhakikisha salamu ziawafikia wapangaji wote waliopangishwa na chama hicho kwenye uchaguzi uliopita .

Munisi alisema kuwa ifike mahali washindani wao wanadi sera na kuacha manung’uniko yasio na lazima kwani chama kilichopo madarakani kimeendelea kuwaletea wananchi maendeleo na kutekeleza ilani ya uchaguzi uliopita kwa asilimia kubwa hivyo sasa ni wakati wa kukamilisha yale  yaliobakia .

CREDIT: WOINDE SHIZZA!

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO