Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA KASKAZINI WAZINDUA MPANGO WA KUCHANGIWA FEDHA KWA NJIA YA SIMU ZA MKONONI

Na Ferdinand Shayo, Arusha.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini kimezindua rasmi mpango wa kuchangia chama hicho kupitia simu za mkononi ili kukiwezesha chama hicho kushinda katika Uchaguzi mkuu wa taifa utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za mkoa za chama hicho ,Katibu wa Chadema kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amesema kuwa michango itakayokusanywa na wanachama na wapenzi wa chama hicho itawawezesha kufanya kampeni nchi nzima na kuikomboa nchi hii kwa kupata viongozi bora.

Golugwa alisema kuwa kutokana na watanzania wengi kuchoshwa na uongozi mbovu wa CCM wanahitaji kukichangia chama hicho ambacho ndicho tumaini la pekee kwa Watanzania la kuleta mabadiliko ya kweli.

“Hatutaki tushindwe kufanya kampeni kwasababu hatuna fedha hivyo tunawaomba wanachama na mashabiki wa chama hicho kukichangia chama hicho kupitia simu zao za mikononi kwa kupitia namba maalumu tutakayowapatia” Golugwa

Alisema kuwa mpango huo umeanza rasmi na unakubalika kwa mujibu wa sheria za usajili wa vyama vya siasa kuwa chama kitapata mapato yake kupitia michango mbali mbali kwa wanachama.

Katibu huyo wa Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amewataka polisi na vyombo vya usalama pamoja na tume ya uchaguzi kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa misingi ya haki na ukweli hasa katika kipindi ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi ili kuepuka kuhatarisha amani.

“Tusifanye masihara na amani ,tunahitaji tume huru na yenye uadilifu itakayofanya kazi yake vizuri bila kuegemea upande wowote” Alisema Golugwa

DSC_0118

KATIBU CHADEMA KAS

Katibu wa CHADEMA kanda ya Kaskazini Amani Golugwa akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Uzinduzi wa mpango wa
kuchangia Chadema kwa kutumia simu za mikononi kukiwezesha chama hicho
kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Picha na Ferdinand Shayo

MATUKIO MENGINE YA SIKU HIYO KONG’OLI HAPA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO