Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KAMPENI: Chadema wasafiri kwa chopa kusaka majimbo Kanda ya Ziwa

Mawazo

Mwenyekiti wa CHADEMA Geita, kamanda Alphonce Mawazo akizungumza na wananchi wa Nyatukala Sengerema katika ziara ya chama chake Kanda ya Ziwa, ziara inayotambulika kma “Operesheni Tigi Tigi”

*********

Mwanza

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Ziwa Magharibi, kimeanzisha operesheni maalumu kwa ajili ya kusaka ubunge katika majimbo yote yaliyoko kwenye kanda hiyo ambayo yanashikiliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Operesheni hiyo inayojulikana kama ‘tigitigi’, ilianza juzi kwa kutumia usafiri wa helikopta katika majimbo kadhaa, ikiwamo Jimbo la Sengerema linaloshikiliwa na mbunge wa sasa, William Ngeleja.

Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Geita Alphonce Mawazo ni miongoni mwa makada wa chama hicho waliofika katika jimbo la Sengerema juzi, wakiambatana na kada wa chama hicho anayetaka kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo hilo,  Hamis Tabasamu.

Akihutubia kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika vijiji tofauti kwa muda wa dakika 30 katika kila kijiji, Mawazo alisema wameanzisha operesheni hiyo kwa lengo la kushinda ubunge kwenye majimbo yote yaliyoko kwenye kanda hiyo ili kuleta ukombozi wa kweli kwa wananchi.

“Wananchi naomba niwambie tumeanza na Jimbo la Sengerema, tutapambana hadi hatua ya mwisho ili kulikomboa jimbo hili. Tunataka Kanda ya Ziwa iwe ya mfano, tutazunguka kata zote na vijiji vyote katika mikoa ya Geita, Simiyu, Mwanza, Tabora, Shinyanga na Mara kuelimisha wananchi,” alisema Mawazo na kuongeza’

“Pia naomba wananchi  mjitokeze kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura ili tuweze kupata nafasi ya kufanya mabadiliko ya kweli mwezi Oktoba. Ndugu zangu mapambano yameanza hakuna kulala, huu ni wakati wetu Chadema,” alisema.

Naye mtangaza nia wa jimbo hilo, Hamis Tabasamu ambaye aliwahi kuwa diwani wa Sengerema, alisema kuwa watafungua ofisi 78 za Chadema kwenye jimbo hilo ili wananchi waweze kuwa na sehemu za kutoa malalamiko yao kwa viongozi na kuhudumiwa.

Alisema muda uliopo sasa ni wa kufanya mabadiliko na kwamba kazi ya kutafuta ukombozi Sengerema imeanza, hivyo ni jukumu la wananchi wa eneo kuunga mkono jitihada za chama hicho za kuwaletea maendeleo endelevu.

“Mimi ni mtangaza nia wa jimbo hili nipo tayari kushirikiana na nyie kuleta mabadiliko ya kweli Sengerema. Tutafungua ofisi 78 hapa na kazi zitafanyika kila kona ya jimbo hili ili tuweze kuing’oa CCM hapa. Nia na sababu ya kuing’oa CCM tunazo kwa kuwa ni ukweli kwamba haijafanya kitu chochote katika uongozi wake eneo hilo,”alisema Tabasamu.

CHANZO: MWANANCHI

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO