Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Uandikishaji Wanachama 'Tanzania Bloggers Network' (TBN), 22/04/2015

new002

Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' - TBN 

kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika 

ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania 

wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.

Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa 

mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka kujiunga fomu hizo zinapatikana 

kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo 

mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha 

mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- 

ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa 

kulipa shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa siku za kazi kuanzia 

saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, 

Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu 

na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili. 

Kwa wanachama wa mikoani utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo mara moja na wanachama 

watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN. Utaratibu unafanywa kupata viongozi wa 

kanda wa muda watakaoratibu usajili kwa kushirikiana na viongozi wa muda wa TBN taifa. Viongozi wa 

muda wa mikoa na kanda watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu zoezi la kujiunga 

uwanachama wa TBN. 

Mikoani TBN itagawanyika kwa kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya Tanga na Pwani 

yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Nyanda 

za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini (jumuisha 

mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Morogoro na Singida), 

Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa), Kanda ya Ziwa (yenye mikoa ya Kagera, 

Geita, Mara na Mwanza), na Kanda ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na 

Manyara).

Kwa wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama wa TBN utafanyika kwa 

muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili kutoa fursa kwa viongozi na kamati husika 

kutathmini wanachama waliopatikana na litafunguliwa tena baada ya miezi sita.

NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy hiyo wataigharamia 

wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za 

TBN. 

Imetolewa na:

Joachim Mushi, 0756469470 

Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO