Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF HAMAD MAHAKAMANI KISUTU!

 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Maalim Seif Shariff Hamad (mwenye suti ya kijivu)akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam, akisikiliza kesi inayomkabili wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Liipumba na wenzake 30 wakituhumiwa kufanya mkusanyanyiko usio halali.

****

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad leo amehudhuria katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba na wenzake 30 wa chama hicho.

Maalimu Seif alifika na msafara wake wa magari matatu Mahakamani hapo majira ya saa nne asubuhi.

Hakimu wa Makakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Cyprian Mkeha amesema washitakiwa hao wanadaiwa kufanya kosa la jinai la kufanya mkusanyiko usio halali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Hakimu huyo ametoa dhamana kwa watu wote kutokana na maelezo yao kama masharti ya dhamana yalivyokuwa yakihitajika.

Hakimu huyo, amesema kuwa kesi inayomkabili Profesa Lipumba na wenzake 30 ni ya kufanya mkusanyiko usio halali kwa mujibu wa sharia za nchi mnamo januari 22 na 27 maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam na upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.

Jopo la mawakili wa kesi hiyo likiongozwa na Wakli,Job Karario awali walipeleka pingamizi la mashtaka dhidi ya Profesa Lipumba na wenzake 30.

Hakimu Cyprian aliahirisha kesi hiyo mpaka itakapotajwa tena Mei 6 mwaka huu na washitakiwa wote katika kesi hiyo wamepewa dhamana.

(Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii)

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO