Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BILIONEA DANGOTE AKAGUA UFUKWE ATAKAOJENGA BANDARI YAKE YA KISASA MTWARA


Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Alhaji Dangote akipata maelezo kuhusu eneo alilopewa na Serikali ya Kijiji cha Mgao lenye ukubwa wa heka 2500 sawa na hekta 1000. Anatarajia kuanza kujenga bandari hiyo mapema mwaka huu.

Msafara wa Alhaji Dangote ukitoka eneo atakalojenga bandari katika Kijiji cha Mgao

Ndege iliyomleta Dangote ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara tayari kwenda kukagua eneo atakapojenga bandari yake.

Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti

Dangote akilakiwa na Esther Baruti

Alhaji Dangote akilakiwa na Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Majanbu

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akisalimiana na Alhaji Dangote

Alhaji Dangote akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (kushoto) Mwakilishi wake hapa nchini, Esther Baruti na Balozi Dk, Majanbu

Alhaji Dangote akizungumza na Esther Batuti

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dedengu akimtambulisha Alhaji Dangote kwa wananchi alipowasili katika Kijiji cha Mgao, ambapo amepewa Dangote  eneo la ujenzi wa Bandari

Alhaji Dangote akisaini katika kitabu cha wageni alipowasili katika Kijiji cha Mgfao kukagua eneo la ujenzi wa Bandari pamoja na kiwanja alichopewa na wanakijiji kujenga makazi yake.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Abdulrahman Shaa

Wananchi wakiangalia msafatra wa Alhaji Dangote uliokuwa unakwenda eneo asmbapo bandari itajengwa.

Alhaji Dangote akiwa na viongozi wa Kijiji cha Mgao pamoja na wananchi akikagua uwanja heka mbili na nusu aliyopewa kwa ajili ya kujenga makazi yake katika kijiji hicho

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja aliopewa  na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na miradi mingine ya maendeleo.

Msafara wa Alhaji Dangote ukielekea eneo patakapojengwa Bandari


Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa akihojiwa na wananchi kuhusu maufaa watakayopata wanakijiji endapo Nadari hiyo ikijengwa

Alhaji Dangote akizungumza na wanahabari kuhusu ujenzi wa bandari hiyo


Msafara wa Dangote ukitumia magari kutembelea kiwanda cha saruji kinachojengwa






Alhaji akijadiliana jambo na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha saruji, Kushoto ni Paschasia Ngaiza Mama Mzazi wa Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais wa Tanzania, Premy Kibanga ambaye pia alikuwepo kwenye ziara hiyo.

Alhaji Dangote akizungumza na Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Majanbu muda mfupi kabla ya kuondoka jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akimuaga Alhaji Dangote uwanjani hapo

Alhaji Dangote akiteta jambo na mwakilishi wake hapa nchini, Esther muda mfupi kabla ya kupanda ndege kwenda Ethiopia na hatimaye Lagos, Nigeria.

Alhaji Dangote akiaga

Dedengu akijadiliana jambo na Esther

Balozi wa Nigeria nchini, akizungumza jambo na Dendengu pamoja na Esther. Kulia ni Paschasia Ngaiza

Ndege iliyombeba Alhaji Dangote na ujumbe wake ikiondoka Uwanja wa Ndege wa Mtwara

 

STORI NA PICHA SOURCED FROM VIJANA NA MATUKIO (JEFF MALIBENEKE)

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO