Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BBC Swhili: Rais wa Nigeria ni Muhhamadu Buhari; Jonathan Akiri Kushindwa

Nigeria

Rais mteule was Nigeria Jenerali Muhammadu Buhari

********************

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria,INEC, Attahiru Jega amemtangaza rasmi Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria jenerali Muhammadu Buhari kuwa rais wa taifa hilo kubwa barani Afrika baada ya kumbwaga rais wa zamani Goodluck Jonathan.

Tayari rais anayeondoka madarakani Goodluck Jonathan amekwisha kubali kushindwa kwake baada ya kumpigia simu mpinzani wake, Jenerali Buhari na kumpongeza kwa ushindi huo wa kihistoria.

Hii inakuwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa rais wa nchi hiyo kung'olewa madarakani na kiongozi wa upinzani.

Goodluck amekiri kushindwa katika uchaguzi huo ulioshuhudia ushindani mkali

Wadadisi wa maswala ya ndani wanasema kuwa inaonekana kuwa Nigeria sasa imekomaa kisiasa haswa baada ya kushuhudia mapinduzi kadha ya kijeshi tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1960.

Hata hivyo kumekuwa na taharuki kubwa haswa baada ya tume ya uchaguzi kuchelewa kutoa matokeo ya uchaguzi.

Hofu ingalipo kuwa huenda wafuasi wa wagombea hao ambao wanatofautia kimsingi katika maswala kadha ikiwemo ya kidini na vile vile kimajimbo .

Wanigeria wengi wamefurahi kushiriki uchaguzi uliomtoa mamlakani raisl aliyekuwa hatekelezi wajibu wake

Wanigeria wengi wamefurahi kuwa hatimaye wameweza kuing'oa mamlakani serikali ambayo haikuwa ikitekeleza majukumu yake kikamilifu.

Buhari angali hajatangazwa rasmi kuwa mshindi na tume hiyo japo alikuwa amefungua pengo la zaidi ya kura milioni tatu dhidi ya mpinzani wake wa karibu rais Goodluck

 

CHANZO: BBC SWAHILI

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO