Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

FAMILIA YA EDWARD MORINGE SOKOINE WAFANYA MISA YA KUMKUMBUKA BABA YAO

unnamed

Familia aliye kuwa waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine wakiwa katika ibada maalumu ya maadhimisho ya kifo chake  nyumbani kwake monduli juu, siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka

Wake wa  aliye kuwa  waziri mkuu  wa Tanzania  hayati Edward Moringe Sokoine  , wakiweka  mashada ya maua kwenye kaburi la  mume wao nyumbani kwake eneo la monduli Juu wilayani monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake siku ambayo huadhimishwa April 12 kila mwaka.

Watoto wa kiume wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Joseph Sokoine,Tumaini Sokoine na Ibrahimu Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake jana.

Watoto wa kike wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Kutoka kushoto:  Maria Sokoine,Joyce Sokoine ,Mbunge wa Viti Maalum Namelock Sokoine na Seki Sokoine wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao nyumbani kwake eneo la Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya kifo chake jana.

Mbunge wa Viti Maalum, Namelock Sokoine akiwa na kaka yake ibrahim Sokoine katika kumbukumbu ya kifo cha baba yao aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Mbunge wa Viti Maalum na Mtoto wa  aliye kuwa waziri mkuu  wa zamani   hayati Edward Moringe Sokoine, Namilock Sokoine akiongea na baadhi ya wazee wa kimaasai baada ya misa maalumu ya maadhimisho ya kifo  cha Sokoine amabayo yalifanyika  nyumbani kwa marehemu eneo la Monduli juu wilayani Monduli mkoani Arusha jana.

Mbunge wa viti maalu, Namelock Sokine akizungumza na wadau 

 

PICHA&STORI: Mroki Mroki

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO