Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BAVICHA Mbeya Walaani kitendo cha Jeshi la Polisi Kuwakamata vijana wa Red Brigade wa Tunduma na Kuutangazia Umma kuwa Wamekutwa na Silaha za Kivita Wakidai Sio Kweli

BARAZA LA VIJANA (BAVICHA) MKOA WA MBEYA

Tarifa kwa umma,
Bavicha tunalaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mkoani hapa kuwakamata vijana wa Red Brigade wa Tunduma na kuutangazia umma kuwa wamekutwa na silaha za kivita jambo ambalo si kweli.
Ikumbukwe siku ambayo Mathew Mwafongo maarufu kama 'Ras' na Salehe Sichalwe walikamatwa na Polisi katika eneo la Sogea Tunduma wakiwa wanajiandaa kwenda Momba Vijijini ndipo askari hao walimkamata na kuwawekea Visu ndani ya gari waliyokuwa wakitumia. Askari hao waliwapeleka kituo cha polisi Tunduma na wakautangazia umma kuwa watu hao ni magaidi jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote.


Kwa nyakati tofauti kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya RPC Msangi alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akiwahusisha vijana hao na ugaidi,Alsha-bab na jana aliutangazia umma kuwa ni majambazi.


Kauri ya RPC Msangi inalengo la kukichafua Chama na Baraza la Vijana ili jamii ione CHADEMA na viongozi wake hawafai mpango ambao umefeli na katu hautaweza kufanikiwa kuidhoofisha harakati za ukombozi katika Mkoa huu.


Tunalaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuendelea kutumika kukihujumu Chama chetu na kuwa kamata na kuwabambikia kesi watu wasio na hatia.
Tunalitaka Jeshi la Polisi kuacha mara moja mchezo wa kukamata vijana wa CHADEMA na kuwapakazia kesi,Bavicha hatutaendelea kuwafumbia macho na badala yake tutachukua hatua zaidi.
Kitendo cha jeshi hilo kuendelea kufanya hivyo ni kujenga chuki miongoni mwa jamii yetu jambo ambalo si zuri sana kwa mustakabari wa taifa letu.
Natoa Rai yangu kwa polisi wote nchini kuwa wafanye kazi kwa weledi huku wakizingatia maadili ya kazi yao na si kutumiwa na Chama tawala katika kukabiri nguvu ya upinzani nchini.
Imetolewa April 27,2015
NA:
GEORGE TITO
MWENYEKITI WA BAVICHA
MKOA WA MBEYA

*******************

Patrobas
Mweyekiti wa Bavicha Taifa, Patrobas Katambi, ambaye ametangaza nia ya Kugombea Ubunge Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA akipata ridhaa.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO