Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Uchambuzi wa Rymond Mtani : ACT-Wazalendo na Zitto

 

Nadhani Zitto atafanikiwa kujenga chama chenye ufuasi na huenda upepo wake ukaleta mtikisiko kwa wapinzani baadaye Oktober.

Nasema hivyo si kwa kuwa ni mwanachama/mfuasi au muumini wa ACT, hasha, bali uwepo wa ACT nauona ukiathiri zaidi upinzani kuliko CCM. Hivyo naitazama UKAWA ikigawana kura na ACT na hivyo kuifaidisha CCM.

KWA NINI ZITTO ATAFANIKIWA.

Zitto atafanikiwa kwa sababu kuu mbili, ya kwanza ni opportunist (mchangamkia fursa) na amekwishafanikiwa kwa kuwa kiongozi mkuu wa ACT jambo alilopigania kwa muda akiwa CDM.

Kufanikiwa kuwa kiongozi mkuu mwenye majukumu zaidi kuliko mwananchama mwingine wa chama chake kunampa fursa ya kutimiza ndoto zake za kupambana kufikia sehemu ya ndoto zake.

Jambo la pili Zitto kwa sasa yuko motivated (amehamasika) ana kitu kinaitwa the Go Power (Nguvu ya kwenda) kitu kinanachompa msukumo wa kutenda zaidi ili kupata zaidi.

Nguvu hiyo inastawisha dhamira yake ya kuwaonesha wakosoji wake kuwa anaouwezo wa kuanzisha jambo na likawa kwa kiwango kikubwa kuliko matarajio yao.

muhimu tu ni kuwa kazi ya siasa ina mambo yake ambayo kabla hujaamua kufanya siasa wapaswa kuyaelewa. Je, unaingia katika siasa kufanya biashara? au unaingia kupambana ili kukomboa kile kinachoitwa "wanyonge".

Ili kujua nani anafanya biashara na nani anafanya ukombozi zingatia mambo haya:-

1. Ukiona mtu anafanya jambo la kijamii na likafanikiwa na baadaye akalitumia jambo hilo kupata fursa nyingine ya kisiasa au kijamii basi elewa tu huyo ni mfanyabiashara wa kisiasa kwa maana aliwekeza na mtaji wake ilikuwa kutenda jambo hilo ili baadaye apate faida ya kisiasa.

2. Mwanasiasa mwenye lengo la ukombozi uwe wa fikra, uchumi, demokrasia, uadilifu nk huubiri uzalendo na kuhamasisha watu na nafsi yake hudhihirisha hilo kupitia matendo yake ya awali ya sasa na matarajio yake kamwe hawezi kutaja taja "mimi ni Mzalendo" "mimi mzalendo" matendo yake huonesha uzalendo pasi na yeye kutumia matendo yake kuelezea uzalendo wake.

3. Akitamka kuwa ni mzalendo maana yake anafanya biashara, na uzalendo ndiyo kauli ya mauzo kwa mantiki hiyo anahitaji faida binafsi kupitia mauzo husika yaani (UZALENDO).

4. Ukiona anakwambia mimi ni mpambanaji nilifanya A,B, C na hivyo nastahili fursa tena jua tu yuko kazini kufanya biashara. Ukiumizwa sana unaweza muuliza tu kwa majuku yako hiyo kazi ulofanya alipaswa kufanya nani?

zittoZitto akihutubia wananchi wa Iringa jana
**

Nilikwisha sema siku za nyuma na ningali na msimamo wangu kuwa Uzalendo ni "imani", na imani bila matendo imekufa....ukiwa mwema na mcha Mungu huitaji kubeba biblia/au Msaafu kutangaza kuwa u Mcha Mungu bali matendo yako ya asili, ya kila siku, maono yako, maongezi yako nasaba zako bila kujali wewe ni imani gani yataonesha u mtu mwema na watu watasema hakika huyu ni mcha Mungu.

Vivyo hivyo Ukiwa mzalendo huitaji kulipia matangazo kudhihirisha uzalendo, ili twende sawa tuangalie mifano ya wazalendo walio hai na hawasikiki wakitagaza uzalendo wao badala yake kazi zao zimekuwa chachu ya watu wengine kuwasemea na kukili kuwa ni wazalendo.

1. Jaji Msitaafu Joseph Sinde Warioba ambaye pia ni wazir mkuu mstafu kazi zake mbili ya kwanza inayotangaza uzalendo wake kwa taifa ni matpkeo ya tume aliyoiongoza kwa ajili ya kutafuta suruhu ya RUSHWA INCHINI mwishoni mwa miaka ya 1990. Ya pili ni ile ya Juzi kuhusu maoni ya wananchi yaliyozaa rasim mbili za katiba kabla ya hii inayopendekezwa. Binaafsi sikuwahi kusikia kwa kinywa chakeakitamba kuwa mimi ni mzalendo, badala yake hujikita kuchambua mambo mengine.

2. Mzee Makweta (Marehem) Waziri wa zamani wa Elimu, yeye na tume yake walizunguka dunia nzima kutafiti mfumo wa elimu uliyofaa kwa ujenzi wa taifa mwanzoni mwa miaka ya 1980, pamoja na kuwa matokeo yake hayakufanyiwa kazi ilivyostahili asilimia kubwa ya maboresho ya sera ya elimu ya mwaka 1995 yalitokana na kazi ile huyu hakuwahi kutangaza uzalendo wake.

3. Harrison Mwakyembe na tume ya bunge ilochunguza sakata la Richmond pamoja na makandokando yake hajatumia hoja hiyo kutangaza kuwa yeye ni mzalendo kwa sababu aliangusha serikali.

Nadhani nikiishia hapa sio dhambi karibu kwa mjadala.

11073849_825367277555655_4578147914463732641_n

Kikatuni cha wachora katuni kikionesha hali kama ya moto wa upinzania unajaribu kuzimwa

Ray Mtani.

Kinondoni Dar es Salaam.

 

NB: Picha zote zimewekwa na Blog hii kutoka mitandao ya kijamii

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO