Cake maalum iliyoandaliwa kwenye sherehe za uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa uliofanyika mwishoni mwa juma kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins kabla ya zoezi la kuwasha mishuma 70 kwenye cake hiyo ikiwa ni uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Mshehereshaji wa sherehe hizo Afisa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins wakiwa wamejumuika na wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye mnuso huo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiwasha nakshi nakshi zilizowekwa kwenye cake maalum ya uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini. Anayemkingia upepo ni walioandaa Cake hiyo kutoka kampuni ya M.E Gift Wraps and Delivery huku Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins naye akijianda kufanya zoezi hilo.
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakishiriki kuwasha mishumaa 70 iliyowekwa kwenye cake hiyo.
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakikata cake kwa niaba ya wafanyakazi wenzao.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akila kipande cha cake kwenye mnuso huo.
Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakilishana cake kabla ya kupata chakula cha usiku wakati wa shamra shamra za uzinduzi wa miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi wenzake.
Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakijumuika kwenye chakula cha usiku wakati wa sherehe za uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akifuatiwa na Afisa Habari wa UNIC, Usia Nkhoma Ledama wakipakua chakula cha jioni kwenye mnuso huo.
Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakijisevia nyama choma ndani ya hoteli ya White Sands.
BAADA YA KUPATA BUFEE LA NGUVU ULIWADIA ULE WASAA WAKUFANYA DIGESTION YA CHAKULA KWA KUSAKATA RHUMBA...
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakisakta rhumba kwenye hafla ya uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakionyesha ufundi wa kusakata rhumba kwenye mnuso huo.
Kwa picha zaidi bofya link hii
0 maoni:
Post a Comment