Basi la kampuni ya Urio Safaris lenye namba za usajili T 137 BCX inayofanya safari zake kati ya Moshi na Leguruki mkoani Arusha leo limepinduka katika eneo la Kia na kujeruhi watu zaidi ya 31.
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio walisema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa basi hilo kujaribu kukwepa pikipiki iliyokuwa imeingia barabarani kwa ghafla.
"dereva huyu alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki ndipo gari ikamshinda na kuhama barabara ndipo ilipo anguka gafla na kubiringita mara tatu. Hapa yenyewe unavyoiyona tumeigeuza ilikuwa kichwa chini matairi juu" alisema mmoja wapo wa shuhuda ambaye akutaka kutaja jina
Mpakamtoa taaifa anaondoka eneo la tukio watu 31 walikuwa wamekwishwa pelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Hai kwa ajili ya matibabu wakiwemo wanafunzi wa shule ya Leguruki ambao walikuwa wanarejea shuleni mara baada ya kumaliza likizo yao ya sikukuu ya Pasaka.
Wananchi wawakiwa wanashuhudia ajali hiyo iliotokea leo jioni katika eneo la kia ambapo inasemekana watu zaidi ya 31 wamejeruliwa
Picha ya chini na juu ni baadhi ya majeruhi walikuwa kwenye basi hilo aina ya Urio lililopata ajali leo jioni katika eneo la Kia Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro
PICHA ZOTE NA: LIBENEKE LA KASKAZINI BLOGU
0 maoni:
Post a Comment