Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa maelezo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kumkabidhi Tuzo ya Heshima ya Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa ziadi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 aliyoipokea kwa niaba ya Mhe. Rais Kikwete tarehe 9 Aprili, 2014 Jijini Washington D.C, Marekani. Heshima hiyo kwa Rais Kikwete ilitolewa na Jarida Maarufu la Kimataifa la African Leadership Magazine Group.
Mhe. Rais Kikwete na Wajumbe wengine waliokuwepo akiwemo Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Bw. Salvatory Rweyemamu wakimsikiliza Mhe. Membe.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membekupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe.
Mhe. Membe akimkabidhi rasmi Mhe. Rais Kikwete Tuzo yake.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, wakiangalia cheti cha heshima alichopewa na Gavana wa Maryland wakati wa kupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe.
Mhe. Rais Kikwete akionesha Tuzo hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mhe. Membe.Picha na IKULU na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
0 maoni:
Post a Comment