Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Uturuki kushiriki miradi ya ujenzi nchini

 

uturuki_2-300x169KAMPUNI tatu kutoka Uturuki zimeingia nchini kwa lengo la kushiriki katika ujenzi kwenye miradi tofauti katika maeneo mbalimbali.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA ya Uturuki, Orhan Babaoglu, alisema kukua kwa sekta ya ujenzi nchini ndicho kigezo kilichowafanya wafungue ofisi zao.

Akizungumza kwa niaba ya Kampuni ya Bosandra Professional Co. Ltd , Babaoglu alimpongeza Waziri wa Ujenzi, John Magufuli kwa kusimamia sekta hiyo hadi kampuni kutoka Uturuki kufungua ofisi zao nchini.

“Tumekuwa tukifuatilia uendeshwaji na ukuaji wa sekta ya ujenzi katika mataifa mbalimbali barani Afrika na tumejiridhisha kuwa Tanzania  ni nchi inayofanya vizuri katika upande huo,” alisema Babaoglu.

Mwakilishi  mwingine wa Kampuni ya CEYTUN, Kursat Durak, alisema utendaji wa kampuni kutoka Uturuki unafahamika duniani  kote, hivyo ujio wao una lengo la kuamsha ushindani wa ubora lakini pia kuona gharama za utekelezaji wa miradi hiyo zinadhibitiwa kwa kuwa na washindani kutoka maeneo tofauti.

Waziri Magufuli alisema hivi sasa kuna miradi mbalimbali inayokusudiwa kuendeshwa kwa kushirikiana na sekta binafsi, hivyo ni fursa kwao pia kuangalia maeneo yatakayowavutia.

Na Lucy Ngowi, Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO