Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: DIWANI NANYARO AKAGUA KUKAMILIKA KWA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO KATA YA LEVOLOSI

Mh Ephata Nanyaro Diwani wa Kata ya Levolosi akipokea maelezo toka kwa Dk Naaman Hosea Mtaalamu wa Upasuaji na Uzazi kuhusu chumba cha upasuaji, vifaa vitakavyokuwepo na huduma nzima ya uzazi. Kulia kabisa ni Injinia wa Manispaa anayehusika na ukaguzi wa Majengo, Engineer Samwel

Mh Ephata Nanyaro Diwani wa Kata ya Levolosi akikaribishwa kukagua Ujenzi, Vifaa na Hadhi ya Hospitali ya Mama na Mtoto Levolosi

Dk Naaman Hosea Mtaalamu wa Upasuaji na Uzazi akiendelea kumpa somo Mh. Diwani kuhusu chumba cha upasuaji, vifaa vitakavyokuwepo na huduma nzima ya uzazi.

Dk Naaman Hosea akimwelezea kuhusu chumba cha kupumzikia mama na mtoto baada ya kujifungua kwa upasuaji.

Ukaguzi unaendelea

Wauguzi nao waliendelea na maandalizi ya kuwezesha Hospitali kufunguliwa na Mh. Rais mapema iwezekanavyo

Muuguzi Mkuu wa Jiji, Sister Jeni Bara akimpongeza Mh Diwani kwa kazi yao nzuri ya kuwezesha Jiji kuwa na Hospitali ya Mama na Mtoto

Muuguzi Mkuu wa Jiji, Sister Jeni Bara akimwonyesha ukarabati wa jengo la zamani la mama na mtoto Levolosi

Ukarabati wa jengo la zamani la mama n mtoto Levolosi unaendelea vema. Kutoka kushoto; Engineer Samwel Mshuza, Diwani Nanyaro na Muuguzi

PICHA ZOTE NA MAELEZO:  DANIEL URIOH

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO