Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mabomu tena Arusha: Bomu lalipuliwa Bar na kujeruhi makumi ya wahudumu na wateja waliokuwa wakiangalia mechi ya Chelsea.

DSC_0094

Katika kile kinachoonekana kuwa mfululizo wa matukio ya ulipukaji wa mabomu Jijini Arusha, jioni ya jana Aprili 13, 2014 ulitokea mlipuko wa kinachodhaniwa kuwa bomu la kurushwa kwa mkono katika Bar maarufu kwa maonesho ya mechi za mpira wa Ulaya, ijulikananyo kama Arusha Night Park aka M.T.K Bar iliyopo maeneo ya Mianzini na kujeruhi zaidi ya watu 20 wengi wao wakiwa wateja waliojazana kushuhudia mpambano baina ya Chelsea na Swansea City za Englanda majira ya saa moja na nusu jioni.

Majeruhi walikimbizwa hospitali za Mt Meru na Dr Mohamed kwa matibabu ya haraka, na hakuna taarifa rasmi ya mtu aliyepoteza maisha ingawa baadhi ya walionusurika wanshuhudia kuwepo watu waliokatika miguu.

Taarifa ya awali kutoka Jeshi la Polisi inaeleza kuwa bomu hilo ni la kutengenezwa kienyeji baada ya kukuta vipande vya vyuma na misumari eneo la mlipuko. Aidha taarifa zaidi zinaeleza kuwa bomu hilo lilirushwa na mtu anayeendelea kusakwa na Jeshi la Polisi likiwa kwenye mfuko wa plastiki kuelekea katikati ya mashabiki hao.

Bado haijaweza kufahamika sababu hasa za zilizopelekea mlipuko huo ingawa kuna watu wenye hisia tofauti, baadhi wakidhani ni maswala ya ushindani wa kibiashara na wengine wakihisi huenda ni maswala ya kisiasa ama utalii.

Pamoja na hayo, Mkuu wa Mkoa Mh Magessa Mulongo amewataka wakazi wa Arusha kuwa watulivu katika kipindi hiki wakisubiri taarifa rasmi ya kilichotokea na kuahidi kuwa Jeshi la Polisi litafanya uchunguzi na kubaini wahusika.

Tukio hili limetokea wakati Jiji hili bado lina kumbukumbu ya matukio matatu mengine ya mshambulizi ya bomu  katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi lililopo Olasiti na shambulio lingine katika mkutano wa Chadema uwanja wa Soweto wakifunga kampeni za udiwani Juni 15, 2013, ambapo takribani watu sita waliuwawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa vibaya huku baadhi wakipoteza viuongo. Tukio jingine ni la Usa River wakati wa mkesha wa mwaka mpya ambapo akina mama kadhaa waliokuwa wakitoka kanisani walirushiwa bomu lililoelezwa kutoka kwenye gari la Polisi waliokuwa doria usiku huo na kuumizwa vibaya miguuni.

DSC_0093Sehemu ambayo ndipo bomu hilo lililipuka na kusambaa ikiwa imeanza kufanyiwa uchunguzi na wataalamu wa mabomu. DSC_0095

DSC_0092

DSC_0096Baadhi ya wananchi waliofika eneo la mlipuko kutaka kujua na kushuhudia kilichojiri

IMG-20140414-WA0005

IMG-20140414-WA0006

IMG-20140414-WA0007

IMG20140414WA00001

Picha hizi tatu juu japo ni hafifu lakini zinaweza kuonesha baadhi ya majeruhi wa mlipuko huo, kwa hisani ya mdau Chris Nnko

DSC_0090

DSC_0091

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO