Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KIKWETE AFUNGUA RASMI OFISI MPYA YA TRA MJINI KARATU; CHADEMA WAMPONGEZA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunu kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kufungua rasmi ofisi ya Mamlaka ya mapato Wilaya ya Karatu leo mjini Karatu.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mbumge wa Karatu mchungaji Israeli Nase(Watatu kushoto),Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe(Wapili kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo(kushoto) na Mkurugenzi wa Utumishi na utawala wa TRA aliyemwakilisha Kamishna mkuua wa TRA Bwana Abubakari Kunenge(wapili kulia) na kulia ni mwakilishi wa ofisi ya TRA Mkoa Bi.Caroline Ntinku.

***********************************

RAIS Jakaya Kikwete amesisitiza msimamo wa Serikali, kwamba mashine za elektroniki za ukusanyaji kodi (EFDs), lazima ziendelee kutumika nchini. Alisema hayo jana wakati alipozungumza kwenye uzinduzi wa Ofisi za Mamlaka ya Bandari (TRA) mjini Karatu katika Mkoa wa Arusha, na kuongeza kuwa changamoto za mashine hizo zinajadilika.

“Najua kuna maneno mengi kuhusu suala hili. Kwa hiyo maelekezo yangu ni kwamba kaeni chini, mjadili matatizo yaliyopo na kupata ufumbuzi. Kama ni suala la bei pia linazungumzika lakini tunahitaji mfumo huu wa malipo ya kodi,” alisema.


Aliagiza viongozi wa TRA kukaa chini na wadau na watumiaji wa mashine hizo kuzungumza na kutafuta majawabu yanayolalamikiwa na wadau.

Alisema kuacha kutumia mashine hizo ni kurudi nyuma kwa kuwa zimeshaanza kutumika duniani kote na hata nchi jirani baadhi zimeshaanza kutumia na nyingine ziko katika maandalizi ya kutumia.

“Kwenye hili tusirudi nyuma kwa sababu tukifanya hivyo, tutakuwa tunarudi nyuma sana kwa sababu dunia nzima inaelekea huko na hata majirani zetu wote ama wameanzisha mfumo huo ama wanajiandaa kuuanzisha.”

“Hatuwezi kurejea kwenye mfumo ule wa kutumia vijirisiti. Mfumo wa sasa unaifanya kazi ya kukusanya kodi kuwa rahisi kwa Serikali yenyewe na kwa walipa kodi. Najua watu hawapendi kulipa kodi lakini hakuna njia ya jinsi ya kuendelea isipokuwa kwa kulipa kodi,” alisisitiza Rais Kikwete.

Kwa muda mrefu TRA imekuwa ikisisitiza kuwa utaratibu wa kutumia mashine za EFDs ulianzishwa kwa lengo la kumrahisishia mfanyabiashara utunzaji wa kumbukumbu za biashara za kila siku pamoja na kuondoa usumbufu wakati wa ukadiriaji wa kodi. Mfumo huo wa kutumia mashine za kodi za kielektroniki ulianza kutekelezwa kwa awamu.

Awamu ya kwanza ilianza mwaka 2010 kwa wafanyabiashara waliosajiliwa kwenye kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Awamu ya pili ilianza 2013 ikiwahusu wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa kwenye VAT ambao mauzo ghafi kwa mwaka ni Sh milioni 14 na zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa za TRA, wafanyabiashara zisizo rasmi zikiwemo za mama lishe na wale wanaotembeza bidhaa barabarani, hawahusiki kwa sababu hawana sehemu maalumu ya kufanyia biashara.

Miongoni mwa wafanyabiashara wanaotakiwa kutumia mashine hizo ni wenye maduka ya vipuri, mawakili, maduka ya jumla, wafanyabiashara wakubwa wa mbao, migahawa mikubwa, maduka ya simu na vipuri vyake, baa na vinywaji baridi, studio za picha, biashara za kutoa huduma za chakula, wauzaji wa pikipiki, maduka makubwa ya nguo na biashara zinginezo Kwa mujibu wa taarifa za TRA, kwa nchi nzima walengwa ni wafanyabiashara laki mbili tu kwa awamu ya pili kati ya wafanyabiashara zaidi ya milioni moja na nusu ambao wamesajiliwa kulipa kodi.

Rais Kikwete alikuwa katika ziara ya siku moja kukagua shughuli za maendeleo wilayani Karatu katika Mkoa wa Arusha na jana na leo ameanza  ziara kama hiyo ya siku moja katika Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro

CHADEMA WAMPONGEZA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Karatu kimeeleza kufurahishwa kwake na mchango unaotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika kuchochea maendeleo bila upendeleo.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilisema kuwa pongezi hizo zilitolewa jana mchana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Lazaro Titus Massey wakati wa sherehe za uzinduzi wa jengo la Halmashauri hiyo mjini Karatu.
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inaongozwa na Chadema.

“Ni lazima tutoe shukurani kwako kwa sababu bila wewe kuwa Rais wa Tanzania, sisi Karatu tusingepata jengo hili.
Pamoja na kwamba Halmashauri yetu ni Chadema bado umeamua kuchangia maendeleo ya wilaya yetu kwa kuchangia kiasi kikubwa ujenzi wa jengo hili. Sisi hata robo ya fedha za ujenzi huu hatukuweza kuzitoa,” alisema Massey huku akishangiliwa na wananchi.

Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Karatu limegharimu Sh1.412 bilioni na kati ya hizo, Serikali imetoa Sh1.394 bilioni na halmashauri imechangia Sh18 milioni.

Rais Kikwete alisema sera ya Serikali yake ni kusambaza maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali misimamo yao ya kisiasa wala kuongozwa na hisia nyingine mbali na ukweli kuwa kila mtu anataka maendeleo.

 

CREDIT: WOINDE

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO