Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NEWS UPDATES: ASKARI WA JESHI LA POLISI NA WENZAKE 4 WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA KWA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imewahukumu kifungo cha miaka 30 kila mmoja aliyekuwa askari wa Jeshi la Polisi na wenzie wanne wakituhumiwa kwa unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akisoma hukumu hiyo mahakamani hapo  Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alisema watuhumiwa wote kwa pamoja wanatiwa hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi wawili.

Alisema ushahidi uliotolewa na shahidi wa kwanza ambaye alikuwa dereva Ezekia Matatira (34) na shahidi wa pili  Sreedhar Pasupelet(38) mwenye asili ya Kiasia kwamba haukuacha shaka yoyote na ulishabihiana.

Awali Mwendesha mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa akisaidiwa na Basilius Namkambe alisema washtakiwa wote kwa pamoja  wanatuhumiwa kwa kosa moja la unyang’anyi wa kutumia Silaha kinyume cha Sheria kifungu cha 287 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mulisa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mshitakiwa namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye namba F8302, 

Elinanzi Mshana(22)Mkazi wa Iyela Jijini Mbeya, Askari Magereza mwenye namba B 500 Sajenti Juma Mussa(37) wa Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29) Mkazi wa Iyela na Amri Kihenya(38) Mkazi wa Iyela.

Alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 3, Mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya Mbeya Chunya.

Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kulizuia gari aina ya Pick Up lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34) Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sreedhar Pasupelet(38) mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo mawili ambayo ni GX 100 Toyota Cresta T 782 BEU na Gari lingine ambalo lilikuwa na namba za Chesesi GX 6011832 aina ya  Grand Mark II.

Kwa upande wake Wakili wa utetezi, Ladilaus Lwekaza, aliiomba mahakama kuwapunguzia hukumu washtakiwa kwa kile alichodai watuhumiwa bado ni vijana na hawana rekodi ya makosa ya nyuma.

Aliongeza kuwa washtakiwa wote kwa pamoja wanafamilia zao ambazo zinawategemea hivyo wapewe adhabu ndogo ili waweze kuzitumikia familia zao pamoja na taifa kwa ujumla.

Kutokana na maombi hayo Hakimu Mteite hakukubaliana naye na badala yake alisema kwa mojibu wa sheria kutokana na kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha washtakiwa walipaswa kwenda jela miaka 30 pamoja na viboko.

Aliongeza  kuwa adhabu ya viboko ameifuta kutokana na mshtakiwa namba mbili kujeruhiwa kwa risasi wakati wa tukio hivyo watasamehewa wote kwa pamoja ila watatumikia kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja.

 

Kutoka kushoto ni mshitakiwa wa pili Elinanzi Eliabu Mshana, Mshtakiwa wa nne Mbaruku Hamis, Mshita

kiwa wa tatu Juma Mussa ambaye aliyekuwa Askari Magereza kwa Cheo cha Sajini , Anaefuatia ni Mshtakiwa wa kwanza PC James aliyekuwa Askari Polisi Wilaya ya Mbeya, na wa mwisho ni Mshitakiwa wa Tano Amri Kihenya .

Washitakiwa wanne kati ya watano kutoka kushoto juu hadi wa nne wakiwa wanatoka mahakamani chini ya ulinzi mkali.

Moja ya Gari lililotumika kufanya uharifu wa unyang'anyi wa kutumia silaha

Ulinzi ulinzi mkali uliimalishwa mahakamani hapo

Na Mbeya yetu

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO