Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TAHA Kuwakutanisha Wakulima na Wafanyabiashara wa Bidhaa za Kilimo 500 kutoka Kanda ya Kaskazini na Taasisi 48 za Fedha April 25&26 Jijini Arusha

WAKULIMA na wafanyabiashara za kilimo zaidi ya 500 kanda ya kaskazini mwa Tanzania wanatarajiwa kukutanishwa na taasisi za kifedha 48 ili kuweza kuongeza ufahamu na uelewa juu ya huduma mbalimbali za nkifedha zitolewazo na mabenki,taasisi ndogo ndogo za kifedha,mashirika ya bima,taasisi za elimu na mashirika yasiyo ya kiserikali.


Akizungumza na vyombo vya habari afisa mtendaji mkuu wa TAHA bi.Jackline Mkindi amesema kuwa wakulima wadogo wadogo wamekukwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya ya upatikanaji wa huduma za kifedha hususani kwa wadau wa sekta ya kilimo.


Katika kutatua changamoto hiyo ya mitaji Agri-Hub Tanzania ikishirikiana na TAHA mashirika,asasi mbalimbali kwa umoja wao wamethamiria kuwaunganisha wadau wa kilimobiashara na watoa huduma za kifedha moja kwa moja ili pande zote mbili ziweze kukuelewana na juu mahitaji yao na hatimaye watoa huduma za kifedha waweze kubuni huduma bora zaidi za kuimarisha utoaji huduma zao kwa wadau wa kilimo.


Mkindi alisem kuwa maonesho hayo yatakwenda sambamba na uwasilishwaji wawa mada mbalimbali ikiwemo uaandaaji bora wa wa mpango biashara (business plans),umuhimu wa wa soko la hisa katika kuhakikisha upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu na matumizi bora ya mikopo katika biashara hususani za kilimo.


Naye mtaribu kutoka kampuni ya Agri-Hub Tanzania bw,Tom Ole Sikar,alisisitiza kuwa maonesho hayo yanalenga kuwawezesha wakulima wajasiriamali pamoja na wamiliki wa biashara za kilimo kama wachuuzi,wauzaji wa pembejeo na wasindikaji kutambua fursa mbalimbali za mitaji na usalama wa kifedha(Financial security) zilizopo kwa biashara za kilimo.


Aidha sikar alisema kuwa wadau hao wataweza kuunganishwa na taasisi muhimu za fedha ikiwa ni pamoja na kushiriki katika mawasilisho na majadilino juu ya fursa za sekta binafsi katika kilimo pamoja na wataalamu wa mambo ya fedha na watoa huduma za maendeleo ya biashara kupitia semina zitakazotolewa sambamba na maonesho hayo.


‘’maonesho hayo yatawawezesha wadau kutambua njia za kuboresha biashara na utoaji wa huduma kwa walengwa ikiwa ni pamoja na kujifunza kutoka kwa wafanyabiashra wengine wa kilimo waliofanikiwa kutembelea maonesho “alisema bw,Sakar


Maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Taasisi ya AVRDC(The World Vegetable Centre) kuanzia tarehe 25 na 26 april kuanzia majira ya saa tatu aubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.

Mkurugenzi wa Tanzania Horticulture Association(TAHA)  Bi Jackline Mkindi akizungumza na vyombo vya habari ambao hawapo pichani juu ya maonesho ya kilimo ambao yanatarijiwa kufanyika siku ya Aprili 25 na 26 katika viwanja vya AVRDC vilivyopo eneo la Tengeru Wilayani Arumeru mkoani Arusha. Kulia kwake ni Mratibu wa Agri-Hub Tanzania Bw,Tom ole Sika

 

Waandishi wa habari wakiwa wanafatilia taarifa iliyokuwa  inatolewa na afisa mtendaji mkuu wa Taha

CHANZO: LIBENEKE LA KASKAZINI

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO