Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwigulu Nchemba akacha sherehe za Muungano zilizompeleka Marekani na kwenda kufunguwa tawi la CCM

Huku akiendelea kutafuna pesa za masikini walipa kodi jijini Wshington D. C. , Mh. Nchemba ameacha sherehe za muungano ambazo kilele chake kilikuwa leo Jumapili April 27, 2014 kwa mpambano kati ya Zanzibar vs Tanganyika na kwenda kufungua tawi la wanawake District of Columbia, Maryland na Virginia (DMV).

Mshangao mkubwa ulikuwa ni pale ambapo Mh. Mwigulu alikuwa amealikwa kama mgeni rasmi ambaye alipaswa kutoa kombe kwa mshindi na medali kwa timu zote mbili. Mwigulu alikuwepo tang mechi inaanza na alifanya ukaguzi wa team zote mbili. Alikuwepo pia wakati kipindi cha pili kinapo anza, lakini haikujulikana alitoweka muda gani. Kwa kutawaliwa na uchama na kuweka utaifa pembeni, aliwaacha balozi Mulamula na waTanzania solemba uwanjani huku akikimbilia shughuri za chama. Ilibidi Balozi na afisa mwingine watoe medali kwa wachezaji badala ya Mwigulu aliye uacha utaifa hapo uwanjani na kukimbilia uchama

      Wachezaji na waTanzania wengi wameonyesha masikitiko ya kuachwa mataa na kiongozi huyu hapo uwanjani bila kujua hatima ya kukabidhi kombe na medali. Wengi ya waTanzania hapa DMV wamekuwa wakihoji kuwa huyu jamaa, Mwigulu, ujio wake hapa USA ulikuwa muariko wa kufunguwa tawi la wanawake DMV au sherehe za muungano. Kwa bahati mbaya maafisa ubalozi walio ulizwa swali hili walimung'unya maneno na swali lilienda bila jibu.

Swali ambalo halina jibu hadi hivi sasa kwa wana DMV: Ujio wa Mh. Mwigulu DMV, USA ulikuwa kufungua tawi la CCM wanawake au sherehe za muungano?

KATIKA HATUA NYINGINE, MWIGULU ALIKUTANA NA WAKATI MGUMU JANA PALE ALIPOKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI MAREKANI WALIOMHAKIKISHIA KUIDAI TANGANYIKA WAKIWA NI WAUNGAJI MKONO WA RASIMU YA TUME YA RAIS YA KATIBA

10300419_629623820453846_528013402052803013_n

10155277_629623777120517_2902360482730161041_n

10174826_629623730453855_2854909969837298521_n

 

Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha sana, Mwigulu aliongea maneno ya dharau sana na ubabe kwa watanzania hao kama VIDEO HII inavyothibitisha.

Alipo kutana na waTanzania na Wazanzibar nchini Marekani ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington D. C. , April 26, 2014 Mh. Nchemba alikana kuwepo kwa Tanganyika na kusema hakuna kitu kama hicho. Alisistiza afadhari angekuwa mzee labda tungetarajia afe ndio Tanganyika irudi, lakini kwa kuwa kijana; tutasubiri sana hadi Tanganyika irudi.  Kwa kifupi Mh. Nchemba amesema Tanganyika hairudi yeye akiwa hai.  Haya majigambo ya huyu muheshimiwa yanathibitisha kauli yake kuwa, kurudi kwa Tanganyika ni "over my dead body"

 

SOURCE: CHADEMA DIASPORA

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO