Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAMEYA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAUURI NA MAJIJI WAKUTANA ARUSHA

Wito umetolewa kwa Halimashauri zote nchini kutafuta njia mbadala za kuongezea Mapato yake ya ndani tofauti na ilivyizoeleka kutegemea mapato yatokanayo na ushuru mbalimbali wanaokusanya katika halimashauri zao.

Wito huo umetolewa jana na mkuu wa ya wilaya ya Arusha John Mongela wakati akifungua mkutano mkuu wa asasi ya umoja wa majiji Tanzania TACINE inaowakutanisha wakurugenzi pamoja na mameya wa majiji tanzania uliofanyika mkoani hapa.

Alibainisha kuwa watendaji wa halimashauri zote hapa nchini wanatakiwa kuangalia namna ya kuleta maendeleo katika halimshauri zao kwa kuunda miradi mikubwa yenye tija ambayo inaweza kukuza mapato ya halmashauri zao

Washiriki wa mkutano mkuu wa TACINE wakiwa wanamsikiliza mgeni rasmi akiwa anafungua mkutano

Mwenyekiti wa TACINE  Atanasi Kapunga akiongea katika mkutano huo

Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela Akiwa anafungua rasmi mkutano wa umoja wa majiji  TACINE  uliofanyika jiji Arusdha hivi leo

Picha na Bertha Mollel

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO