Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Ukawa sasa yapania kufanya ziara nchi nzima; Yaaanza na Mkutano mkubwa Jijini Mwanza jana

IMG-20140331-WA0017Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akihutubia wananchi wa Jiji la Mwanza jana masuala mabalimbali kuhusiana na Bunge la Katiba ikuhusisha Umoja wa Katiba ya Wananchi. Tayari kwa nyakati tofauti CCM kupitia Katibu Mkuu wake wamekwishafanya mikutano kama hiyo na kuendesha makongamano Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CUF nae alifanya hivyo wiki iliyopita Visiwani Zanzibar
IMG-20140331-WA0021Baadhi ya viongozi wa UKAWA mkutanoni hapo

Viongozi wakuu wa UKAWA wakitoa taarifa kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wiki jana. na kueleza kwamba Muungano wa Vyama vya Upinzani (Ukawa) nje ya Bunge la Mabadiliko ya Katiba (BMK), unajiandaa kuzunguka nchi nzima kufanya kampeni ya kuelimisha umma juu ya ukiukwaji wa haki na kanuni za Bunge hilo unaofanywa na chama tawala.

Wakitoa tamko la pamoja kwa waandishi wa habari jana, Makatibu Wakuu wa Vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, Dar es Salaam walisema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimekuwa kikijihusisha na vitendo vingi vinavyokiuka kanuni za upatikanaji wa Katiba Mpya ikiwamo utoaji wa rushwa kwa baadhi ya wajumbe.

“Ukawa-nje tumepata taarifa ya kutolewa kwa ahadi za vyeo baada ya Bunge kwa baadhi ya wajumbe ili kuunga hoja sera za CCM,” sehemu ya tamko ilieleza kupitia kwa Dk. Willbrod Slaa.

Ukawa-nje, wanasema kuwa hata hotuba ya Rais licha ya kuonekana kuipinga rasimu iliyosomwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba iliweka wazi dhamira ya CCM kupitisha mapendekezo yao.

Katibu Mkuu wa Chadema alimpongeza Profesa Ibrahim Lipumba kwa ujasiri wake wa kukataa uongozi ndani ya BMK, ingawa kuna posho za ziada kwa kuwepo katika nafasi hiyo.

“Wingi wa wana-CCM ndani ya Bunge isiwe hoja ya kuvuruga utaratibu mzima na wanatakiwa wajue kuwa Watanzania walio nje ni wengi zaidi yao,” alisema Dk. Slaa.

Naye Mkurugenzi wa Habari wa CUF (Taifa), Abdul Kambaya alisema kuwa wajumbe wa Ukawa waliunga mkono uchaguzi wa Samuel Sitta kuliongoza Bunge hilo kutokana na uwezo wake aliounyesha wakati akiwa Spika wa Bunge lililopita, lakini isiwe sababu ya CCM kutumia fursa hiyo kama faida kwao.

“Uongozi wote wa juu wa bunge umeshikwa na watawala ambao hawawezi kuzalisha katiba nzuri ya wananchi,” alisema Kambaya.

Wajumbe hao pia walieleza kuwa utungaji wa Katiba ni suala la hoja, ushawishi, mijadala huru, maafikiano na maridhiano. Kwa kuwa mpaka sasa taifa limeshatumia zaidi ya Sh81 bilioni katika mchakato huo ni vyema kanuni zikazingatiwa.

Ukawa-nje wanaanza ziara yao leo (jana) katika Jiji la Mwanza kuhamasisha wananchi kuwa makini na mwenendo wa BMK. Ziara hizo zinaweza zikawakosa wenyeviti wa vyama hivyo, ambao nao ni Wajumbe wa BMK wanaoendelea na vikao mjini Dodoma.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO