Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MABOMU YAIZINDUA POLISI ARUSHA, YAWATAKA WAMILIKI WA KUMBI ZA STAREHE KUFUNGA KAMERA ZA CCTV

JESHI la Polisi limewataka wafanyabiashara wakubwa hasa wamiliki wa kumbi za starehe jijini Arusha na Halmashauri zake zote kuhakikisha wanafunga mitambo ya kamera (CCTV CAMERA) kwenye maeneo ya biashara ili iwe rahisi kuwabaini wanaotaka kusababisha milipuko ya mabomu.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja mara baada ya watu wasiofahamika kutega bomu katika nyumba ya kulala wageni ya Arusha Night Park, huku bomu lingine likiwa limetegwa katika baa nyingine ya Washington Baa mapema juzi.

Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mngulu, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya usalama wa Mkoa wa Arusha kutokana na kukumbwa na milipuko ya mabomu ya mara kwa mara.

Alisema hadi sasa takwimu zinaonesha kuwa matukio hayo yanajirudia, hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kuanzia sasa kwani hata mabomu ya kienyeji nayo yanatumika sana kuua na kujeruhi.

Alisema hata uongozi mzima wa Mkoa wa Arusha nao unatakiwa kuhakikisha kuwa kuanzia sasa unaanza mikakati ya kufunga vifaa mbalimbali ambavyo vitakavyoweza kuwabaini wahalifu wote wa mabomu kwani uwezekano wa kuwatambua hata kupitia vifaa hivyo upo.

Aliongeza kuwa wamiliki wa kumbi za starehe nao pia wachukue tahadhari kuanzia sasa ambapo wanatakiwa kulinda uhai wa wateja wao na kamwe wasijisahau, hivyo wanahitajika kuwa na vifaa vya kisasa hasa CCTV CAMERA ili kuharakisha zaidi upelelezi.

"Kutokana na hali ya mabomu ilivyo kwa sasa ni muhimu sana kwa kila mtu kuchukua tahadhari ingawaje na sisi tutahakikisha tunawalinda ipasavyo wananchi wetu na hatutaweza kuruhusu tena Arusha ikapatwa na janga lingine la mabomu, ingawaje pia tunaimarisha ulinzi kila kona hususan kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu," aliongeza Isaya.

Katika hatua nyingine alisema kuwa Jeshi la polisi nchini limetangaza kitita cha milioni 10 kwa mtu yeyote atakayewezesha kutoa taarifa sahihi na kukamatwa kwa mtuhumiwa aliyesababisha mlipuko wa bomu katika nyumba ya kulala wageni (Arusha Night Park)

Wakati huo huo, Polisi mkoani hapa wameahidi kuimarisha ulinzi zaidi wakati wa Sikukuu ya Pasaka ambapo watatumia vifaa mbalimbali ili kuweza kuepusha jamii na milipuko ya mabomu.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema kuwa ulinzi katika maeneo yote ya mikusanyiko ya watu utakuwa wa kutosha na hivyo jamii haipaswi kuwa na woga wala hofu ya aina yoyote ile

Sabas alisema watatumia vifaa mbalimbali kuimarisha ulinzi kwenye mikesha na mikusanyiko ya watu kuanzia siku ya Ijumaa Kuu hadi Pasaka. "Tutatumia rasilimali watu, farasi, mbwa na nyinginezo na hii ni kutokana na kuwa tunataka wananchi waweze kusherehekea siku hiyo kwa amani na utulivu," alisema.

CHANZO:  GAZETI MAJIRA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO